Home SPORTS TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI KUIKABILI BENIN.

TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI KUIKABILI BENIN.

Na: Stella Kessy DAR.

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars leo Oktoba 4 kimeanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Kikijiandaa na mchezo utakaochezwa Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa katika kuwania  kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia wakiwa wapo kundi J.

Hata hivyo mpaka sasa kiungo wa simba Jonas Mkude bado hajaripoti katika mazoezi ya  kutokana na matatizo ya kifamilia kwa mujibu wa Meneja wa Stars, Nadir Haroub.Hata hivyo Kocha mkuu  Kim Poulsen amewapatia wachezaji   program maalumu wachezaji wote ili kuwaweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.

Pia Kibu Denis na Kibwana Shomari ni miongoni mwa wachezaji ambao wameripoti kambini leo na kuanza mazoezi Uwanja wa Mkapa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here