Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw Sabasaba Moshingi,( wa pili kulia) akiongoza zoezi la kugongesha glasi kuashiria upendo na furaha kwa wateja wa benki hiyo wakati hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika leo Jumatano Oktoba 6,2021 katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Diana Myonga.
DAR ES SALAAM.
BENKI ya Biashara Tanzania TCB imesema hatua ya serikali kuweka mifumo imara ya kifedha imezidi kuziboresha huduma za kifedha nchini ikiwemo kuongeza namba ya watu wanaotumia mifumo rasmi ya kifedha.
Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma Kwa wateja Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi amesema Nia Yao ni kutoa huduma hasa kuwapa fursa wateja wadogo wadogo ambao ndiyo azma ya Serikali na Benki hiyo ya Biashara ya Tanzania
Moshingi amesema kuwa nia yao nikusogeza huduma rafiki kwa wateja wake ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania wa hali ya chini anatumia benki hiyo kwaajili ya uendeshaji wa biashara zao katika Nyanja tofauti.