MBUNIFU nguli wa mavazi nchin Ally Rehmtula, amendaa onyesho la mavazi Sunset Festival, kwa wahitimu ambao alikuwa akiwapatia mafunzo ya ubunifu kwa muda wa miezi mitatu.
Onyesho hilo ambalo anashirikiana na Manispaa ya Kinondoni litafanyika October 14 katika ufukwe wa Coco beach ikiambatana na kumbukumbu ya miaka 22 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julia’s Kambarage Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema katika onyesho la Sunset Festival, nguo zitakazo onyeshwa zimetengenezwa na wanafunzi wake tisa ambao amekua akiwapatia mafunzo.
“Nimekuwa na darasa kwa vijana ambao wanapenda kuwa wabunifu huu ni msimu wa pili wa mafunzo haya katika shoo ya Sunset Festival, mavazi ambayo yataonyeshwa yametengenezwa na wahitimu ambao pia tuta watunukia vyeti vyao,” alisema Ally Rehmtula.
Kuelekea jukwaa la Sanset Festival kutafanyika usahili ufukwe wa Coco beach Oktoba 9 wa wanamitindo ambao watatumika kuonyesha mavazi yaliyo buniwa na wabunifu hao.
“Tunafanya usahili kwa wanamitindo (Models) wa kike na kiume kwa ajili ya kuonyesha mavazi majaji katika usahili watakuwa wahitimu wenyewe kwa sababu wao wanafaham wanataka watu wa aina ipi”