Waziri Bashe ameitaka Taasisi hiyo kuhakikisha inashirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na wadau wengine ili kuteketeza magugu ambayo yamekuwa yakisambaa karibu nchi nzima yanayosababisha uharibifu wa ardhi ya kilimo na ufugaji.
Kikao kikiendelea katika ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI).
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Baraka Sendeka Mchambuzi wa Viatilifu katika maabara za Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha alipokuwa akitoa maelezo kuhusu moja ya mashine zinazotumika kufanya utafiti wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinavyofanyika , Kushoto ni Dkt. Efrem Njau Kaimu Mkurugenzi wa (TPRI).
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Dkt. Efrem Njau Kaimu Mkurugenzi wa (TPRI) wakati akitembelea katika maabara za Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha alipokuwa akitoa maelezo kuhusu moja ya mashine zinazotumika kufanya utafiti wakati alipotembelea Taasisi hiyo kulia ni Jaquiline Mkindi Aisa Mtendaji Mkuu wa TAHA.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Venace Kasenene Mchambuzi wa Viuatilifu katika maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinafanyika katika taasisi hiyo.
Moja ya majengo ya taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akisisitiza jambo wakati akizungumza alipokuwa akitembelea maabara za Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) nje kidogo ya jijini Arusha wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kiutafiti zinavyofanyika katika taasisi hiyo kutoka kushoto ni Dkt. Efrem Njau Kaimu Mkurugenzi wa (TPRI), Ndeninsia Meena Mchambuzi wa Viuatilifu katika maabara na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA Jaquiline Mkindi.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akimsikiliza Bw. Tano Hangali Mkuu wa Kitengo cha Utunzaji wa Viuatilifu na Mazingira TPRI wakati akielezea namna ya kutuza viuatilifu na mazingira katika njia bora.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akizungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo mara baada ya kufanya ukaguzi katika maabara kulia ni Profesa Elinangaya Kweka Mkurugenzi wa Utafiti (TPRI).
Picha mbalimbalizikionesha baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika kikao hicho wakimsikiliza Mhe.Naibu Waziri Hussein Bashe hayupo pichani.