Home LOCAL WAZIRI BASHUNGWA ATOA MIEZI MITATU KITUO CHA AFYA KIBONA KIKAMILIKE

WAZIRI BASHUNGWA ATOA MIEZI MITATU KITUO CHA AFYA KIBONA KIKAMILIKE

Silvia .A. Mchuruza, Karagwe, Kagera
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ameonesha hali ya kutoridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa Kituo cha Afya Kibona.

Kutokana na hali hiyo, ametoa miezi miwili kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kuhakikisha anasimamia ukamilishaji wa Kituo cha Afya Kibona ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo Julai 18, 2022 wakati wa kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Kibona kilichopo kata ya Kanoni Wilaya Karagwe.
Alisema hajaridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa majengo katika kituo hicho.

“Katika taarifa mmeniambia mmefikia asilimia 95 lakini ukiangalia kwa uhalisi sio kweli bado hamjafikia, kwa hiyo natoa miezi miwili kwa ajili ya ukamilishaji ili Serikali ilete vifaa tiba na wananchi waanze kupata huduma,” amesema Bashungwa.

Amesema tayari Serikali imetoa Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa Kituo cha Afya Kibona ili kiweze kuwahudumia wananchi wa Tarafa ya Kanoni na maeneo ya jirani.

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuendelea kuchangia miradi ya maendeeo ambapo wamechangia Sh milioni 17 na nguvukazi ili kuwezesha ujenzi wa Kituo kituo cha Afya Kibona katika Kata ya Kanoni.

Wakati huo huo, Waziri Bashungwa amemuagiza Meneja wa TARURA Wilaya Karagwe kufanya matengenezo kipande cha barabara kinachoingia kwenye Kituo hicho kuanzia barabara kuu ili iweze kupitika kwa urahisi.

Halmashauri ya Wilaya Karagwe ilipokea Sh milioni 500 kwa awamu mbili kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kibona ambapo awamu ya kwanza walipokea Sh milioni 250  kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara na kichomea taka.
Previous articleAPONGEZA JITIHADA ZA WIPO KUENDELEZA UBUNIFU
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 19,2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here