Home LOCAL RC HAPI AIPONGEZA TEMESA KUJENGA ENEO LA ABIRIA MWALO WA MIGOBERO MUSOMA

RC HAPI AIPONGEZA TEMESA KUJENGA ENEO LA ABIRIA MWALO WA MIGOBERO MUSOMA

RC Hapi akizungumza na wananchi alipofika kwenye Mwalo wa Mwigobelo mjini Musoma, kukagua ujenzi wa kivuli na vyoo kufuatia agizo lake la Agosti Mwaka huu.

Mmoja wa wananchi, Shaban Makulile, akishukuru na kupongeza aina ya utendaji kazi wa RC Hapi ambapo alisema hakutarajia kumuona akirudi kuhakikisha kama maagizo yake yametekelezwa na ikiwa taratibu, sheria na kanuni zimezingatiwa.

Na: Mwandishi wetu,Musoma.

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amepongeza Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kwa kuanza ujenzi wa eneo la abiria kupumzikia na vyoo kwenye Mwalo wa Mwigobero mjini Musoma.

Hata hivyo RC Hapi hakuafikiana na taarifa iliyotolewa na Kaimu Meneja wa TEMESA wa Mkoa huo, Vitalis Bilali, kwamba mpaka ujenzi huo ukamilike utagharimu jumla ya Sh Milioni 89.

“Tundu Moja la choo serikalini linajengwa kea Sh Milioni 1·2 hapa mnajenga matundu manne sawa na milioni 4.8,”alisema RC.

Akishirikiana na Fundi Mkuu wa Mradi huo, Mhandisi Joseph Elias, Hapi alifanya hesabu za haraka na kubaini kuwa gharama iliyotajwa ni kubwa ikilinganishwa na bei halisi za vifaa na ufundi. 

“Ninafahamu michoro na gharama  umeletewa na wakubwa zako,  kawaambie wapitie upya hesabu ili gharama ipungue lakini mradi ukamilishwe kwa wakati huku mkizingatia ubora na thamani ya fedha,” amesema RC Hapi. 

Agosti Mwaka huu, RC Hapi alifanya  ziara kwenye mwalo huo na kubaini  kukosekana kivuli kwa ajili ya abiria kusubiri usafiri pamoja na ukosefu wa huduma za vyoo.

Aliagiza muda wa mwezi mmoja kwa TEMESA kuanza ujenzi wa banda hilo na kuweka huduma zote muhimi kwa wasafiri ikiwamo za vyoo.

Previous articlePROGRAMU YA BENKI YA KCB “VIJANA TUJIAJIRI” KUISHINDA DHANA YA KUAJIRIWA.
Next articleMTIBWA ISITEGEMEE MTEREMKO GEITA: KIVUYO.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here