Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MD WA BOUYGUES YA UFARANSA

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MD WA BOUYGUES YA UFARANSA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa Eric Fleurisson Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa Eric Fleurisson baada ya kumalizika kwa Mazungumzo, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Oktoba 15,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa  Eric Fleurisson Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mzungumzo hayo Eric amesema kampuni  ya Bouygues ina  nia ya kuwekeza katika sekta ya Afya nchini hususan katika Ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa mkoani Dodoma. Aidha, amesema kampuni  hiyo ina uzoefu kwa kutekeleza miradi mikubwa ya  kimataifa katika Bara la Afrika ikiwa imejenga Hospitali katika nchi za Benin, Ghana na Ivory Coast.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amekaribisha uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini na kuongeza kwamba kutokana na Serikali kuhamia mkoani Dodoma, mahitaji mbalimbali yamezidi kuongezeka hasa katika sekta ya afya. Makamu wa Rais amesema  uwekezaji wa ujenzi wa Hospitali yenye  ubora na vifaa vya kisasa utaongeza tija kubwa kwa wakazi wa Dodoma na mikoa jirani.

Previous articleRC MAKALLA: DAR SUNSET CARNIVAL KUPAMBA MOTO COCO BEACH KESHO.
Next articleMAJALIWA: TANAPA, WADAU WA UTALII SHIRIKIANENI KUITANGAZA RUBONDO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here