Home SPORTS KULEKEA MCHEZO WA YANGA NA

KULEKEA MCHEZO WA YANGA NA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na waandishi wa Habari(hawapo pichani)jana ofisini kwake kuhusiana na mchezo wa Ligi Kuu  ya NBC kati ya wenyeji KMC na Yanga utaochezwa kesho katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Na: Muhidin Amri, SONGEA.

KUELEKEA Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Timu ya soka ya KMC  na Yanga zote za Dar  es slaam utakaopigwa  apo kesho katika uwanja wa Majimaji mjini Songea,Serikali mkoani Ruvuma imewataka wapenzi na washabaki watakaofika kushuhudia mchezo huo kuchukua tahadhari  dhidi ya Ugonjwa wa Covid 19.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema  hayo, wakati akiongea na Waandishi wa Habari na viongozi wa Chama cha mpira wa miguu mkoani humo(Faru)ofisini kwake mjini Songea.

Jenerali Ibuge amesema,  Serikali  ya mkoa imefanya maandalizi yote kuhakikisha kuna kuwa na amani na utulivu kwa wapenzi na washabaki  wa ndani na  nje ya mkoa wa Ruvuma watakaokuja kushuhudia mchezo huo, hata hivyo ni vyema wakachukua tahadhari  ili kuepuka kuambukizwa Covid -19.

Ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajapa chanjo,kwenda katika vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kupata chanjo kabla ya kuingia uwanjani ili kujikinga na  kuepuka uwezekano wa kuambukizwa kwa urahisi.

Ameuagiza uongozi wa Chama cha Soka mkoa na Tff kuhakikisha wanaweka vifaa  vyote muhimu ikiwemo  maji tiririka yenye sabuni ambapo kila mshabiki atakayeingi uwanjani  lazima anawe mikono na kuvaa barakoa.

“mchezo huu utachukua idadi kubwa ya watu,kwa hiyo ni lazima serikali tuhakikishe tunachukua hatua ya kudhibiti uwezekano wa watu kupata maambukizi ya virusi vya korona,Tff akikisheni mnaweka vifaa vyote muhimu  na mazingira ambayo rafiki”amesema Ibuge.

 
Aidha Mkuu wa mkoa,amewakaribisha wananchi hususani wapenzi wa mpira wa miguu wa Ruvuma na mikoa jirani ya Nyanda za juu kusini, kuja kwa wingi  kushuhudia mchezo huo utakaoanza majira ya saa tisa jioni na kuwataka watoa huduma kuhakikisha wanaboresha huduma zao kwa wageni.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Ruvuma Kamwanga Tambwe, ameishukuru  Klabu ya KMC kwa kuchagua uwanja wa Majimaji kuwa wa nyumbani na kuhaidi kwamba watatoa ushirikiano  kwa timu hiyo na timu nyingine zitakazo amua kuja kucheza  michezo yake Ruvuma.

Kwa upande wake,katibu wa Timu ya KMC Walter Harson  amesema, wamejiandaa kushinda katika mchezo huo na kuwataka wapenzi wa mpira wa miguu mkoani Ruvuma kuiunga mkono Timu hiyo.

Amesema, katika mchezo dhidi ya Yanga wameweka viingilio rafiki Sh.7000  mzunguko na Sh.10,000  jukwaa kuu ili kutoa fursa kwa watu wengi kwenda kushuhudia mchezo huo.

Pia amesema, baada ya mechi  na Yanga wataangalia uwezekano wa kutumia uwanja wa Majimaji kama uwanja wao wa nyumbani katika mchezo wake na Timu ya Simba ambao utafanyika Mwezi Desemba.
MWISHO.

Previous articleTFS YAKABIDHI MADAWATI 120 SHULE YA MSINGI KIPERA MVOMERO
Next articleRAIS SAMIA AWASILI JIJINI DODOMA BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI MKOANI ARUSHA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here