MWANAMKE mmoja aliyepoteza Jicho,Masikio pamoja na Viganja vya mikono yake miwili baada ya kushambuliwa na fisi wakati akinusuru mifugo yake isiliwe katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ameiomba Serikali kumpatia msaada ikiwa ni pamoja na kuhamishwa kutoka katia eneo hilo.
Rose Kapande (50) Mkazi waa Kijiji cha Esapai kata ya Nainokanoka wilaya ya Ngorongoro ,mkoani Arusha anasema alifikwa na mkasa huo mwaka 2018 ,fisi huyo anayetajwa kuwa na kichaa cha Mbwa pia akifanikiwa kuua Ng;ombe wanne .
Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro linatajwa kama eneo la Uhifadhi Mseto ,masuala matatu yakifanyika kwa maana ya Uhifadhi ,uendelezaji wa jamii inayoishi katika eneo hili pamoja na utalii wakiruhusiwa binadamu jamii ya wafugaji ,Mifugo ,Ng’ombe,Mbuzi na Kondoo kuishi pamoja na Wanyamapori.
Hata hivyo utaratibu huo baadhi ya nyaraka zinaeleza kuwa ulikuwa ni sehemu ya majaribio kuona kama inawezekana ukilenga kutizama uwiano wa mambo matatu kwa maana ya Uhifadhi ,maendeleo ya jamii na utalii.
Changamoto iliyopo sasa kwa wakati huu ni idadi ya watu kuongezeka kutoka 8000 hadi kufikia 100,000 mara 10 zaidi,wakati hiofadhi hii ikianzishwa,mifugo ikiongezeka hadi kufikia Milioni moja kutoka 260,000.
Ongezeko la idadi ya watu na Wanyama limechangia kupungua kwa eneo la malisho pamoja na muingiliano wa wanyamapori na wananchi ambao pia umechangia uwepo wa muingiliano wa magonjwa yanayotoka kwa mifugo,wanyamapori na binadamu.
Matukio mbalimbali ya vifo vitokanavyo na wanyapori kwa binadamu na wakati mwingine kusababisha ulemavu yanatajwa kuchangiwa na ongezeko hili la Binadamu na mifugo .
Rose Kapande mama wa watoto tisa aliyekuwa akiishi peke yake kwenye Boma baada ya kutalikiana na mumewe ni mmoja wa waathirika wa matukio ya kuvamiwa na kisha kushambuliwa na Wanyamapori ,akipoteza viganja vya mikono ,Jicho moja ,Masikio pamoja na fuvu la kichwa .
Mamlaka ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kupitia Naibu Kamishna Mkuu wake Elibariki Bajuta amekiri kutokea kwa matukio ya namna hiyo katika eneo la Hifadhi na kwamba tukio la mama huyo serikali ilifanya jitihada za haraka kuokoa maisha ya mwanamke huyo kwa kuhakikisha anapata matibabu yanayostahili.