Mwandishi wetu Songea.
MABINGWA wa kihistoria Yanga SC leo wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwalaza KMC mabao 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Katika mchezo huo leo ni kiungo wa kimataifa nchini, Feisal Salum Abdallah aliyefunga mabao yote mawili mapema kipindi cha kwanza.
Fei Toto, alifunga bao kwanza dakika ya tano baada ya kufumua shuti kali lililombabatiza mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele kufuatia kudondoshewa mpira na kiungo mwingine, Mkongo Yannick Bangala aliyeuzuia mpira uliookolewa na mchezaji wa KMC.
Hata hivyo bao la pili dakika ya 12 kwa shuti kali pia la umbali wa mita mita 25 baada ya kutengewa pasi na Mayele.
Kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha Mtunisia, Nasreddine Nabi anayesaidiwa kazi na Mrundi, Cedric Kaze ifikishe pointi tisa baada ya mechi tatu za awali, mbili ikicheza ugenini.