Home LOCAL SPIKA NDUGAI AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KULETA MAENDELEO, AONYA...

SPIKA NDUGAI AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KULETA MAENDELEO, AONYA MIGONGANO


Na: Mwandishi wetu, DODOMA.

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali nchini zikiwemo AZAKI yameshauriwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta maendeleo kwani baadhi yao wamekuwa wakitumika katika kuvuruma mipango ya maendeleo huku wengine wakijikita katika kuilamu Seikali kwa jambo ambalo linafanyika.

Ushauri huo umetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wakati akifungua Wiki ya AZAKI iliyoanza leo Oktoba 23 ambayo itakwenda hadi Oktoba 28 mwaka huu katika Jiji la Dodoma, ambapo wadau kutoka mashirika, taasisi za umma na binafsi pamoja na wananchi wa kada mbalimbali wameshiriki.

Akizungumza zaidi Spika Ndugai amesema kuwa anatambua mchango mkubwa ambao AZAKI zimekuwa zikiutoa katika kuchangia maendeleo, lakini ukweli uliopo kuna baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yamekuwa yakitumika katika kuvuruga nchini, jambo ambalo amesema sio nzuri na vema wenye kushiriki mipango hiyo yenye nia ovu kuacha, kwani yanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

“Tunatambua mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na AZAKI zote nchini lakini kuna baadhi yao wamekuwa wakitumika , hawaitakii mema nchi yetu, vyovyote ambavyo watafanya wao ni watanzania tu na lazima tujenge utamaduni wa kuipenda nchi yetu na kuisema vizuri.Wenzetu baadhi yao kila siku wao ni kulalamika tu , wakati mwingine kwa lugha za kejeli na kutukana matusi, hii haiwezekani.Hakuna hata siku moja ambayo wanapongeza, ukiwauliza kwanini wanasema wao wapo kwa ajili ya kukosoa tu, sasa wawe wanajikosoa na wenyewe.

“Pamoja na mambo mengine, niwaombe mtumie Wiki ya Azaki kuweka mikakati itakayowezesha mchango wake katika maendeleo ya nchi yetu, mwenendo ambao baadhi ya mashirika wanakwenda nao ndio unaofanya kuwepo na sheria za kuwabana, ukiomba fedha kwa wafadhili sheria inakutaka utoe maelezo, zinakuja kwa ajili ya nini na zinatumikaje, lakini mkienda sawa na Serikali ni Imani yangu hakutakuwa na sheria ambazo baadhi yenu mnalalamika kuwa zinawabana,”amesema Spika Ndugai huku akisisitiza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ina nia njema na mashirika hayo , hivyo lazima watoe ushirikiano.

Amesisitiza kwamba anachosisitiza katika maelezo yake ni kwamba umefika wakati kila mmoja wetu kuwa mzalendo kwa Taifa hili na kuhakikisha wanatambua mchango wa viongozi kutoka Awamu ya kwanza hadi Awamu ya ha makini katika kufanya mambo yake , anatazama jambo kwa umakini na kisha kutoa maamuzi, tumpe ushirikiano wote kwa umoja wetu,”amesema.


Pia Spika Ndugai amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika Wiki ya Azaki ambayo itakuwa na mambo mbalimbali yatakayojadiliwa huku akitumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa waandaaji hao kuhakikisha wanakuwa na mpango maalumu wa kuwakutanisha wabunge na kisha kuelezea yale ambayo wanayoyafanya, kwani hiyo itasaidia kuwa na muelekeo mmoja kama nchi na wakati huo huo kwenda na muelekezo wa Dunia.

Katika hatua nyingune, Spika Ndugai ametoa ombi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kuungana na Rais Samia katika kuhakikisha wanashiriki katika kuhamasisha kuchanja ili kuzuia athari ambazo zinaweza kutokea katika janga la COVID-19.”Nishauri katika Wiki ya AZAKI kuwepo na banda kwa ajili wananchi watakaofika waweze kuchanja, na bahati nzuri nimeaambiwa tayari banda kwa ajili ya chanjo lipo.”

Wakati huo huo Spika Ndugai ameonesha kukerwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiita wengine mazuzu, kwani sio lugha nzuri na ukweli ni kwamba wao wana akili atimamu akijitolea mfano kuwa yeye sio zuzu na jimboni kwake ameshakuwa mbunge kwa miaka 25 na mara mbili amepita bila kupingwa.”Mimi sio zuzu , ninazo akili, na jimboni kwanu ukija huwezi kupambana na mimi, labda kama unakuja kwa ajili ya kusindikiza”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Wiki ya AZAKI aliyezungumza kwa niaba ya mashirika zaidi ya 20 Lulu Ng’wanakilala ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa wiki hiyo huku akimshukuru Spika Ndugai kukubali kuwa mgeni rasmi.

“Tunakushukuru sana Spika kwani tumefarijika na uwepo wako kwa niaba ya serikali, Kamati ya maandalizi tunasema ahsante na maelekezo yako tumayepokea tu tutashiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo,”amesisitiza.

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovic Otouh ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wajibu amesema mchango wa AZAKI katika maendeleo ni mkubwa na wiki ya AZAKI yam waka 2019 imetoa faida kubwa ikiwemo kuongezeka kwa mijala , na mwaka huu washiriki wa AZAKI mwaka huu walikutana katika kikao cha siku mbili kuangalia mchango wa AZAKI, hivyo kwa kufuata sheria , kanuni na taratibu na kwamba mikakati yao ni kuendelea kuimarisha ushirikiano.


“Tutumie fursa hii mgeni kukuomba uruhusu wabunge wajumuike nasi katika mijadala itakayoendelea kwa juma zima hapa Dodoma , aidha tunawaribisha wananchi wa Dodoma ili wajionee kazi ambazo AZAKI zinafanya, na matarajio yangu katika wiki ya AZAKI ijayo ifanyike nje ya Dodoma ili wananchi wengine nao wanufaike,”amesema.

 ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA AZAKI, DODOMA.


Rais wa Foundation for Civil Society(FCS), Dk. Stigmata Tenga,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu wa Asasi, Mussa Sang’anya,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.


Mkuu wa kitengo cha utawala bora kutoka Ubalozi wa Uswiz Bi.Sacha muller, ,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.


Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano kutoka ubalozi wa Denmark Mette Bech Pilgaard,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.


Kaimu Balozi wa Canada Bi.Helen Fytche ,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.






 

 

 

 

Previous articleHABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO J.MOSI OCTOBA23-2021
Next articleKMC, NAMUNGO ZATOSHANA NGUVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here