NA: MWANDISHI WETU.
Balozi wa Italy nchini Marco Lombardi, amezindua nembo ya msimu wa 14 wa tamasha la mitindo, Swahili Fashion Week ambalo litafanyika kuanzia 3 Desemba mpaka 5 jijini Dar Es Salaam.
Tamasha hili limekuwa likifanyika kila mwaka na kukutanisha wabunifu na wanamitindo kutoka nchi mbalimbali za ndani na nje ya Afrika
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Balozi amesema nchi ya Italy, ipo sambamba na uongozi wa Swahili Fashion Week kuhakikisha wanafanikisha tamasha hilo kwa mara nyengine.
“Imekuwa ni kawaida ya nchi yetu kudhamini tamasha hili kwa sababu tunatambua sekta ya ubunifu wa mavazi inatoa ajira kwa kasi kwa watu wa rika tofaauti kupelekea na kukuza uchumi wetu,” anasema Marco Lombardi.
Kwa upande wamratibu wa jukwaa hilo Benedict Msofe amesema wabunifu Zaidi ya 50 wamejisaji kuonyesha kazi zao mwaka huu katika tamasha hilo.
“Mwaka huu tumepata muamko mkubwa kwa sababu ya wabunifu wengi wamejitokeza kushiriki katika jukwaa hili kuonyesha kazi zao pamoja na kuzi uza katika hoteli ya Serena ambapo ndipo panapofanyika tamasha hili mwaka huu.