Dar-es Salaam, Maonyesho yamefankiwa na yalikuwa yakuvutia kwa kuwa ni jukwaa muhimu ambalo mataifa mbalimbali wamelitumia kwa kuleta bidhaa zao na kufanya na kuonyesha ni namna gani Uwekezaji umekuwa kwa kiasi kikubwa na amewataka Mamlaka ya Biashara Tanzania (TanTrade) wafanye utafiti wa uhakika kubaini masoko mapya ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, na kutoa taarifa hizo kwa Wafanyabiashara ili waweze kuyafikia masoko hayo kwa urahisi
Akizungumza mapema Leo Julai 13 ambapo maonyesho hayo yamefanyika kwa siku16,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi, amesema taasisi zinazosimamia biashara nchini katika serikali zote mbili kuondoa urasimu na katika hilo serikali hizo zitashirikiana kukuza biashara na uwekezaji kwa kufanyia kazi maoni ya wafanyabiashara nchini.
“Wigo wa masoko umepanuka na kutoa fursa ya kufanya biashara na nchi za jumuiya nane za Afrika,Tantrade fanyeni tafiti za uhakika wa masoko mapya ya bidhaa na leteni taarifa kwa wafanyabiashara wazichangamkie, hivyo basi niwaombe Watanzania kutumia fursa ya masoko ya Jumuiya ya Afrika likiwemo soko la Eneo Huru la Soko Afrika (AfCFTA),SADC na la Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya biashara ya bidhaa zinazozalishwa nchini.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis amesema kuwa jumla ya bidhaa zenye thamani ya Sh bilioni 3.8 zimeuzwa wakati wa Maonesho hayo kwa mwaka 2023, ikilinganishwa na sh bilioni 3.6 zilizopatikana katika maonesho ya mwaka jana..
“Jumla ya mikataba tisa ya awali (MOU) imesainiwa katika sekta na maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ununuzi wa pamba uliosainiwa kati ya Bodi ya Pamba ya Tanzania na Algeria kununua tani 30,000 kwa mwaka, na ununuzi wa Mkonge kati ya Bodi ya Mkonge Tanzania na kampuni kutoka India.
Aidha amesema katika maonesho ya mwaka huu yamewezesha kusainiwa MOU katika sekta ya kilimo na elimu na MOU nyingine ni kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Chaudhary Charan Singh Haryana, India kuhusu programu mbalimbali za biashara ya Kilimo, Bioteknolojia, Sayansi ya Chakula.
“kupitia maonesho hayo tumeweza kutoa ajira za muda zipatazo 11,687 na zaidi ya wageni milioni tatu wa ndani na nje ya nchi ni zaidi ya 267 na nchi 17 walitembelea maonesho hayo kupata mahitaji mbalimbali ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo mwaka jana kulikuwa na wageni 265,957”amesema.