Home LOCAL DKT. GWAJIMA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA ALMA

DKT. GWAJIMA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA ALMA

Na.WAMJW- DOM.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo tarehe 05 Novemba, 2021, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Muungano wa Viongozi wa Nchi za Afrika (ALMA) katika kupambana na Malaria, Mama Joy Phumaphi kutoka nchini Botswana.

Katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, kwa pamoja wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya hususani ikiwemo kuanzisha Mabaraza ya Kutokomeza Malaria na  kuanzisha viwanda vya bidhaa za afya hapa nchini zikiwemo za kupambana na ugojwa wa Malaria.

Aidha, kupitia kikao hicho Mama Joy Phumaphi  amesema kuwa ALMA ipo tayari kuwekeza kwenye juhudi za serikali kutokomeza malaria.

Mbali na hayo Mama Joy Phumaphi  ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa namna inavyofanya vizuri katika matumizi ya kadi ya alama juu ya mapambano dhidi ya malaria nchini.

Pia Dkt. Gwajima ameishukuru Taasisi ya ALMA kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchini.

Katika hatua nyingine Mama Joy Phumaphi amepata fursa ya kuonana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ambapo ametoa rai ya ALMA kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa Wabunge wa Tanzania katika Mapambano ya kutokomeza Malaria Tanzania (TAPAMA).

Mwisho.

Previous articleDKT GWAJIMA KUONGOZA MAWAZIRI WENZAKE WATATU KUHUDHURIA MAADHIMISHO WIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA ARUSHA.
Next articleMAWAZIRI WANAOSHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI NA MIPANGO WA NCHI ZA EAC WAKUTANA JIJINI ARUSHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here