Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI MKUTANO WA SADC TROIKA

MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI MKUTANO WA SADC TROIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika), Utatu wa SADC (SADC Troika) na nchi za SADC zinazochangia vikosi vya kijeshi katika nchi za Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao leo tarehe 11 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Stargomena Tax (wa tatu kutoka kushoto), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa (wa tatu kutoka kulia) pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama mara baada ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika), Utatu wa SADC (SADC Troika) na nchi za SADC zinazochangia vikosi vya kijeshi katika nchi za Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao leo tarehe 11 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika), Utatu wa SADC (SADC Troika) na nchi za SADC zinazochangia vikosi vya kijeshi katika nchi za Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji. Mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Mkutano huo umelenga kuangazia hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Kaskazini mwa Jamhuri ya Msumbiji.

Akizungumza katika Mkutano huo, Makamu wa Rais amesema Tanzania inaunga mkono jitihada za kanda za kuimarisha hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kulipongeza taifa hilo kwa utayari wake wa kutoa mchango wa ziada katika uanzishwaji wa Misheni ya SADC nchini humo (SAMIDRC). 

Amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kuchangia hali na mali katika misheni ya SAMIDRC ili kuhakikisha kanda inatimiza malengo yake.

Mkutano huo umeridhia kuongezwa kwa muda wa vikosi vya misheni ya SADC nchini Musumbiji (SAMIM) kwa miezi 12 kutoka Julai 16 2023.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera, Rais wa Msumbiji Felipe Nyusi, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi, Rais wa Zimbabwe Dkt. Emmerson Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi, Waziri Mkuu wa Lesotho Samuel Ntsokoane pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Angola Balozi Te’te Antònio.

Viongozi wengine wa Tanzania waliohudhuria ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Stargomena Tax, Waziri wa Ulinzi Innocent Bashungwa pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Previous articleTIC KUDUMISHA MAHUSIANO YA UWEKEZAJI NA INDIA
Next articleRAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI BARANI AFRIKA KUSHIRIKIANA KATIKA KUPAMBANA NA RUSHWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here