Home BUSINESS MKEMIA MKUU WA SERIKALI DKT. FIDELICE MAFUMIKO ATEMBELEA MABANDA MAONESHO YA 47...

MKEMIA MKUU WA SERIKALI DKT. FIDELICE MAFUMIKO ATEMBELEA MABANDA MAONESHO YA 47 YA KIMATAIFA YA BIASHARA

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akipewa maelezo na Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano BoT, Bi. Noves Moses, kuhusu noti na sarafu za Tanzania. Kulia ni Mhasibu Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sarafu, Bw. Omary Kitojo.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko ( wapili kutoka kushoto) akipewa elimu na Mhasibu Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sarafu BoT, Bw. Omary Kitojo, kuhusu alama za usalama za noti zetu.

Afisa kutoka Tawi la BoT Arusha, Bi. Leah Ombeni, akitoa elimu kuhusu utambuzi wa alama za usalama za noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bi. Joyce Shala, akielezea jambo kuhusu uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Main Greenhill walipotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Afisa Utawala Mwandamizi Bw. Suleiman Tajiri na Bw. Maxmillian Kishiwa kutoka Kurugenzi ya Usimamizi Rasilimali Watu na Utawala BoT wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  

Mchumi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Ujumuishi wa Fedha BoT, Bw. Lucas Magazi, akifafanue jambo kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  

Afisa Uhusiano wa Umma kutoka Idara ya Mawasiliano BoT, Bi. Graceana Mahega, akielezea jambo kwa wananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  

Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha BoT, Bw. Mussa Ambika, akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Dhamana za Serikali kwa wananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania, Bi.Tulla Mwigune, akitoa elimu kuhusu Chuo cha Benki Kuu kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  

Afisa kutoka Idara ya Mawasiliano BoT, Bw. Faki Matauka, akielezea jambo kuhusu utambuzi wa alama za usalama za noti zetu kwa wananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Previous articleTAASISI NDOGO ZA FEDHA ZINAZOKIUKA SHERIA KUCHUKULIWA HATUA – BoT
Next articleZIARA YA MHE. WAZIRI MKUU MKOANI MTWARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here