Home LOCAL DC BULEMBO APITA MTAA KWA MTAA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

DC BULEMBO APITA MTAA KWA MTAA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

Na: Sophia kingimali Dar es salaam

Wananchi wa wilaya ya kigamboni wametakiwa kuongea na watoto kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii ili kumlinda na kumuepusha na vitendo vinavyopelekea mmomonyoko wa maadili ambavyo vimekua vikijitokeza kwenye jamii zao.

Wito huo umetolewa June 19 na mkuu wa wilaya ya kigamboni Halima Bulembo wakati wa ziara yake ya mtaa kwa mtaa inayotekelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo ili kujua na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Bulembo ameanza ziara yake kwenye mtaa wa mkamba uliopo Kata ya kisarawe amesema serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira Bora kuanzia ngazi ya jamii hivyo viongozi katika mitaa na kata wanapaswa kuwasikiliza wananchi na kuwasaidia kwenye changamoto zao.

Aidha Bulembo amesema kuwa ofisi yake inapokea kesi mbalimbali za mmomonyoko wa maadili zinazowahusu watoto zaidi ya mia mbili pamoja na watu wazima zaidi ya miamoja na ishirini hivyo walezi na wazazi wanapaswa kuongea na watoto wao kuhusu maadili Kwani mabadiliko yanaanza na wao katika ngazi ya familia.

Sambamba na hayo Bulembo amewataka wakazi wa mtaa huo kutojihusisha na suala la uhalifu na wafugaji kutolisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima ili kuepukana na migogoro inayojitikeza baina ya wakulima na wafugaji.

Kwa upande wake Afisa mifugo na uvuvi manispaa ya kigamboni Aron Bullu amesema Kuna Sheria mbalimbali za ufugaji ikiwemo mfugaji anatakiwa kua na eneo la ufugaji zaidi ya square MITA nne.

Aidha kwa upande wao baadhi ya Wananchi wameiomba serikali kuwaleta Kwa karibu huduma muhimu kam shule zahanati na kutatua KERO ya umeme wanayokutana nayo.Z

Ziara ya mkuu wa wilaya ya kigamboni inaendelea katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ili kuhakikisha anatambua KERO zinazowakuta wananchi na kuzitatua

Mwisho.

Previous articleTMDA YATANGAZA KUPOKEA KAZI ZA WAANDISHI WA HABARI KUWANIA TUZO MSIMU WA PILI
Next articleRC CHALAMILA AWATOLEA UVIVU WATENDAJI NA MADIWANI, AWATAKA KUACHA KUPOKEA BAHASHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here