Home LOCAL WAPOTEZA MAISHA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI, SIKONGE

WAPOTEZA MAISHA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI, SIKONGE


Na: Lucas Raphael,Tabora

Watu watatu wamefariki dunia wakiwemo watoto wawili na mwanafunzi mmoja  wa shule ya msingi majengo wilaya ya sikonge mkoani Tabora baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba molamu.

Kamanda wa polisi mkoani Tabora akizungumza na waandishi wa habari jana Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea katika kitongoji cha Usenga kijiji cha misheni kata ya misheni wilaya ya sikonge mkoani hapa

Alisema kwamba mnamo Novemba 16 mwaka huu majira ya saa 12 na 30 jioni katika shimo lililokuwa limechibwa na wachina wanaojenga barabara wilayani humo.

Alisema kwamba chanzo ni kuporomoka kwa kifusi /udogo na kuwaangukia marehemu wakati wakiwa chini wakichimba molamu hiyo.

Kamanda huyo wa polisi aliwataja walifariki kuwani mwanafaunzi Rashid Hamis (9) Sadiki Ramadhani (9) na  Bakari Shabani (21).

Aidha aliwataka wananchi wote wa mkoa wa Tabora kuchua taadhari katika maeneo ya ujenzi ambayo kuna mashimo makubwa ili kuepukana na madhara hasa tunavyoelekea katika kipindi masika.

mwisho.

 

 

Previous articleMHE. RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MJUMBE MAALUM WA MASUALA YA BIASHARA WA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA
Next articleHALMASHAURI YA WILAYA TUNDURU YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WANA VIKUNDI WASIOREJESHA MIKOPO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here