Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Wahariri wa Vyombo vya Habari uliofanyika leo June 17, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF), na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Jukwaa hilo, Neville Meena akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi katika mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodatus Balile.Â
MKuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Honoratus Ishengoma, akitoa ukaribisho kwa wahariri wa Vyombo vya habari katika Mkutano wa Sekretarieti hiyo na Wahariri uliofanyika leo Juni 17, 2023 Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bi. Emma Gelani, akitoa mada iliyohusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika mkutano huo.
Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Kipacha, akitoa mada iliyohusu Ukuzaji wa Maadili katika mkutano huo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Anitha Mendoza akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika Mkutano huo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
DAR ES SALAAM
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi, amesema kuwa tasnia ya habari ni Mhimili muhimu unaofanyakazi ya kupokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali na kuzipitia kisha kuzifikisha kwa wananchi kwa lengo la kuhabarisha umma.
Jaji mwangesi ameyasema hayo katika mkutano wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma na Wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika leo June 17,2023 Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yenye kujenga afya katika uwasilishaji wa taarifa kutoka kwenye mamlaka hiyo kwenda kwa jamii.
Amesema anaamini kuwa Wahariri wakielewa vizuri majukumu yanayotekelezwa na Taasisi husika, ni wazi kuwa jamii itafikiwa na taarifa sahihi zilizopitiwa na kuchakatwa kitaalamu.Â
“Tunaamini kuwa ninyi mkielewa vizuri mtaisadia jamii kuielewa vizuri Mamlaka ya taasisi yetu, na mtaitendea haki taaluma yenu na mtazichakata vizuri habari zozote ambazo zitawafikia katika madawati yenu kuhusiana na viongozi wa umma na ukiukwaji wa mahadili kwa viongozi wa umma. Mtazihoji na kuzidadisi taarifa hizo, kuzipembua na kuziangalia matakwa na mazingatio ya Sheria.
“Katika mkutano wetu huu wa leo malengo yetu ni kuongeza ushirikiano kati yetu na nyinyi Wahariri wa vyombo habari ili kutoa taarifa sahihi, kubadilishana mawazo ,kupeana ushuri wenye afya ili kujenga kitu kizuri kutoka kwetu kwenda kwa umma. amesma Jaji Mwangesi.
Nakuongeza kuwa “tunaamini kuwa taarifa zetu zikiwa kamilifu, kupitia kwenu, majukumu na mamlaka yetu kwa mujibu wa ibara ya 132 ya mujibu wa Katiba yetu ya Tanzania wa mwaka 77, na Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995, ambazo ni Sheria tunazozifanyia majukumu yake zitaeleweka vizuri kwa wadau wetu.
“Hivyo ni muhimu kwenu ninyi Wahariri kujua msingi wa mambo muhimu ambayo Taasisi yetu ingependa kuwajulisha viongozi na wananchi kupitia vyombo vya habari” ameongeza Jaji Mwangesi.
Akizungumzia kuharibika kwa Maadili, Jaji Mwangesi amesema sasa hivi suala la Maadili ni kilio kila kona hapa nchini, na kusisitiza kuwa sasa ni jukumu la watu wote kujua namna ya kukabiliana nal tatizo hilo na kulitatua.
“Uadilifu umekuwa ni swala adhimu ikiwemo kwa watoto wadogo wa shule, kwa watu wazima na kwa viongozi ambao ndio linatuhusu. Tunaamini ninyi mna mambo mengi ambayo mnayajua kuhusiana na tatizo hili, hivyo basi mtatujuza na kutushauri kwamba kwa sisi ambao tunahusika na maadili ya viongozi tufanyeje ili kutatua tatizo na kuweza kulipunguza. amesisitiza Jaji Mwangesi.
Kwa upande wake Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili Bw. Waziri Kipacha akitoa mada kuhusu ukuzaji wa maadili, ameeleza kuwa lipo tatizo la vijana kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kuiga mitindo ya maisha ya kigeni na kusahau mila na Desturi za Kitanzania ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kulindwa.
“Huku kwetu huwezi kukuta Kijana anabishana na mtu mzima, lakini kwa wenzetu ni vitu vya kawaida, vijana wanaiga mavazi ya ajabu, wanavaa nguo mpaka wewe unayemuangalia unaona aibu, haya yanaingia huku kwa sababu ya utandawazi ambao kwa sasa upo.
“Mbaya zaidi kuna hili ambalo liliibuka hivi karibuni la ndoa za jinsia moja lakini kutokana na weledi wa viongozi wetu wamelikemea, tunaona kama linapungua pungua kidogo, lilitaka kupata msukumo lakini kama nchi tumesimama kidete kuhakikisha tunalinda Maadili.
(PICHA MBALIMBALI ZA WAHARIRI KATIKA MKUTANO HUO)