Home LOCAL RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  amewateua wafuatao:- 
  1. i) Amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). 
  2. ii) Amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa  Barabara Tanzania (TANROADS). Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi  wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya  Afrika Mashariki (CASSOA). 

Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila  ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu. 

iii) Amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu,  Wizara ya Maliasili na Utalii.  

Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa  ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge na Uratibu); na 

  1. iv) Amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya  Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). 

Uteuzi huu umeanza tarehe 12 Juni, 2023

Previous articleSENYAMULE AAGIZA CHEMBA KUJIPANGA UPYA
Next articleTANZANIA YAZINDUA UBALOZI WAKE VIENNA, AUSTRIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI