Na: Stella Kessy
MABINGWA wa Tanzania bara Simba leo wanashuka dimbani kuchuana na Ruvu shooting katika michunao ya ligi kuu Tanzania bara 2020/2021, katika mtanange utakaopigwa mkoani mwanza katika uwanja wa CCM kirumba.
Kikosi cha simba kinaingia uwanjani kikiwa na jumla ya pointi 11 huku wamecheza mechi 5 na kushinda tatu na kutoka sare mbili huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Yanga wakiwa na point 15.
Mechi ambazo wamecheza Simba dhidi ya Dodona jiji ,Polisi na Namungo kutoka sare na Biashara, Coastal Union.
Michezo mingine leo katika ligi kuu ni Polisi Tanzania watakuwa nyumbani kuchuana na Coastal Unioni, Prison watachuana na Mbeya kwanza,
Kwa upande wa mlinzi wa kati Kennedy Juma amesema anajisikia furaha kucheza katika uwanja ambao ana historia yake ambayo alianza kucheza hapo.
Hata hivyo Kennedy ni mmoja wa wachezaji 24 waliopo katika kikosi na kwaajili y mchezo wa leo.
Kennedy ni ni mwenyeji wa Sengerema amesema anakuwa na furaha kila anapocheza katika uwanja huo.
“Mimi mwanza ni nyumbani tunapoishi si mbali na hapa uwanjani kwa hiyo kila nikifika huku najisikia furaha sana, hata familia yangu huwa inakuja kwa ajili ya kunipa sapoti “ amesema.
Hata hivyo Kennedy amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi leo kwaajili ya kuisapoti timu lengo likiwa ni kuhakikisha wanaondoja na alama zote tatu.
“Nina jua simba ina mashabiki wengi hivyo ninawaomba wajitokeze kwa wingi leo sisi kama wachezaji tumejipanga na tupo tayari kuwapa furaha”amesema Kennedy.