Baraza la Mafamasia na Madaktari nchini yametakiwa kusimamia uandikaji na utoaji wa dawa za antimicrobiatic kulingana na kanuni ya cheti cha dawa.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mfamasia Mkuu wa Seriakli Bw.Daudi Msasi kuelekea maadhimisho ya wiki ya uhamasishaji wa kuzuia Usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya Dawa.
Msasi amesema kuwa Mabaraza ya kitaaluma yana jukumu kubwa katika vita dhidi ya usugu wa dawa hivyo watimize wajibu wao kwa kuzingatia kanuni na taratibu.
Aidha, amewataka wakulima na wafugaji kuacha kutumia dawa kiholela bila ya kupata miongozo ya wataalamu kwani baadhi yao wanatumia vibaya kwa kuwapa mifugo dawa ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
“Dawa za antimicrobiatic ni muhimu lakini zina madhara makubwa endapo zitatumika kinyume na taratibu”.
“Niagize Baraza la famasi na Baraza la Madaktari kusimamia uandikaji na utoaji wa dawa za antimicrobiatic kulingana na kanuni ya cheti cha dawa”amesisitiza Msasi.
Hata hivyo Msasi amewataka wanasayansi na wataalamu katika sekta ya afya kutumia wiki hii ya maadhimisho kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa hizo ili kuzuia madhara yanayosababishwa usugu wa vimelea.
Kwa upande nwingine Mfamasia Mkuu huyo amewataka wafanyabiashara wanaouza mifugo kutotumia dawa za antimicrobiac katika vyakula vya mifugo na mimea.
MWISHO