Wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama walipokua wakiimba wimbo wa taifa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania (TAPSEA) na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mgharibi Idrisa Kitwana Mustafa Akitoa salamu za Mkoa wakati wa Hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania (TAPSEA) na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Makamo wa pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania (TAPSEA) na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA ) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha makatibu mahsusi (TAPSEA) Zuhura Songambele Maganga akisoma risala kwa niaba ya wanachama hao katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka TRAMPA ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Wasanii wakiigiza igizo lenye maudhui ya maadili ya makatibu mahsusi wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka TRAMPA ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Wanachama wa chama cha makatibu muhtasi Tanzania (TAPSEA) na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) wakifuatilia hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa Wanachama hao ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Wasanii wa Mjomba band wakiimba wimbo wenye maudhui ya maadili ya makatibu mahsusi na watunza kumbukumbu wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Waimbaji wa Kwaya wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Wakitoa burudani katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Management ya utumishi wa umma na utawala bora) Goerge Simba Chawene akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Wanachama wa chama cha TAPSEA na TRAMPA Wakila kiapo cha uadilifu na utanzaji wa Siri za serikali wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya wanachama hao huko viwanja vya fumba Zanzibar kiapo hicho kiliongozwa na Wakili wa Serikili Faraji Robet Nguka.
Wanachama wa chama cha TAPSEA na TRAMPA wakijaza hati za kula kiapo wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya wanachama hao huko viwanja vya fumba Zanzibar.
Mkalimani wa lugha za alama akiwasaidia Wanachama wa chama cha TRAMPA wenye mahitaji maalum kujaza hati ya kiapo wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya wanachama hao huko viwanja vya fumba Zanzibar.
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akihutubia katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi wa dini wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar.
Kikindu cha Ngoma ya kibati cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU Wakitoa burudani katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uadilifu na utunzaji wa Siri kwa makatibu mahsusi Tanzania TAPSEA na menejimenti ya watunza kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ambapo kauli mbiu ni “nidhamu,uadilifu na utunzaji Siri za kazi ni chachu ya maendeleo kitaaluma” huko viwanja vya Fumba Zanzibar. Mei 27,2023.
(PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR)
Na: Rahima Mohamed/ Mwashungi Tahir -Maelezo
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka makatibu mahsusi na watunza kumbukumbu na nyaraka kuzingatia miongozo na mipaka ya taaluma zao ili kulinda siri za Serikali.
Rais Samia alitoa kauli hiyo leo wakati akifunga mafunzo ya makatibu mahsusi na watunza kumbukumbu na nyaraka wa Tanzania nzima katikav viwanja vya Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais Samia alisema kazi wanayoifanya kada hiyo ni kubwa na muhimu katika utendaji wa Kazi za taifa na kuwataka kutunza kiapo walichokula ili kuendeleza kazi zao.
“Niwatake mzingatie weledi taaluma zenu na miongozo na mipaka ya kazi zenu kiutendaji. Mmekula kiapo cha uadilifu wakili amewaapisha mimi nikishuhudia kwahiyo mkienda kinyume na kiapo chenu tutajuana mbele kwa mbele,” alisema Samia
Aidha amesema anajua hali za kada hizo kwasababu na yeye alitokea huko alipokuwa Mtunza kumbukumbu na nyaraka na kwamba walisahaulika hivyo anawaahidi kuwanyanyua.
Akizungumzia kauli mbiu ya mkutano huo iliyosema, nidhamu uadilifu na utunzaji siri sehemu za kazi ni chachu ya Maendeleo kitaaluma, Rais Samia alisema sio tu ni chachu bali ni msingi mkuu wa maendeleo.
Alitumia fursa hiyo kuwataka waajiri wanaowauzuia wafanyakazi hao kushiriki mafunzo hayo yanayotolewa kila mwaka, kuwaruhusu kwasababu ndio njia pekee ya kada hiyo kuongeza ujuzi na weledi na kupata njia ya kupumzika kwasababu muda mwingi wanakuwa kwenye majukumu yao tofauti na kada zingine.
Aidha aliwataka mawaziri wanaohusika na utumishi kuzungumza na waajiri wa sekta binafsi kuwapa ruhusa watu hao pindi zinapotokea nafasi za mafunzo .
“Mawaziri mnaohusika zungumzeni na sekta binafsi waachie watu hawa wasiwazuie hii ndio fursa pekee ya wao kutoka nje maana kwa mazingira yao ya kazi hawana muda wa kutoka kama binadamu anatakiwa kupumzika na hii ndio njia yao pekee ya kupumzika, Mawaziri shughulikieni hili,” amesema Rais Samia.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe D.k Hussein Ali Mwinyi Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdulla ameema kada hizo ni muhimu katika utendaji wa kazi kwenye maofisi hivyo kuwataka watendaji kulinda haki zao.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene alisema kada hizo ni injini za ofisi lakini zilisahaulika.
Alisema Chuo Cha Utumishi wa Umma Tabora kimekamilisha mtaala mpya ambao unatarajia kuzinduliwa Julai mwaka huu ambao utasaidia kuwainua kitaaluma.
Wakisoma risala za vyama vyao, walitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kukosa mafunzo na waajiri kuwanyima fursa washiriki hata pale yanapotolewa.
Mwenyekiti wa chama cha makatibu mahususi Tanzania (TAPSEA)Zuhura Songambele Maganga aliomba kiazishwe chombo cha kitaaluma na mafunzo yatolewe hata kwa watendaji wengine kwani wakati mwengine taarifa zinavujishwa na watu wa kada nyengine ambao hawana taaluma za utunzaji wa kumbu kumbu .