Home LOCAL MULUGO KULIPA WALIMU 11 MISHAHARA WANAOJITOLEA SEKONDARI YA NAMALAJI

MULUGO KULIPA WALIMU 11 MISHAHARA WANAOJITOLEA SEKONDARI YA NAMALAJI

 Mbunge wa Jimbo la Songwe, Mhe. Philip Mulugo.

 

Na Thobias Mwanakatwe

 

MBUNGE wa Jimbo la Songwe, Mhe. Philip Mulugo, ameahidi kutoa Sh.330,000 kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa mshahara walimu 11 wanaojitolea katika Shule ya Sekondari ya Namalaji iliyopo kata ya Totowe wilaya hapa.

Aidha, Mhe. Mulugo ameahidi kutoa Sh.milioni 3 mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili ya kununulia photocopy mashine ambayo itasaidia walimu wakati wanapotunga mitihani.

Mulugo alichukua uamuzi huo baada ya kutembelea shule hiyo na kuelezwa na wanafunzi kuwa shule hiyo ina walimu watatu tu walioajiriwa na serikali lakini walimu 11 wanafundishi kwa kujitolea.

Wanafunzi hao walimweleza Mhe.Mulugo kuwa walimu hao wanaojitolea wamekuwa wakilipwa kwa wazazi kuchangishana Sh.6,000 lakini hata  hivyo baadhi hawatoi fedha hizo.

Kufuatia hali hiyo, Mhe. Mulugo alisema ataanza kutoa Sh.330,000 kila mwezi kulipa mshahara walimu hao wanaojitolea wakati wanasubiri ajira kutoka serikalini.

Alisema fedha hizo atakuwa akizituma kila mwezi kwa diwani wa kata ya Totowe ambaye naye ataziwasilisha kwa Mkuu wa Shule hiyo na yeye kuwagawia walimu hao.

Shule ya Sekondari ya Namalagi ilianzishwa January 17, 2022.

Previous articleKUELEKEA SENSA 2022: JE, HAKI YA WANANCHI KUPATA TAARIFA IMETIMIZWA?
Next articleWAZIRI NDALICHAKO AHIMIZA USHIRIKI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here