Katika kusheherekea Maadhimisho ya miaka Sitini ya Uhuru STAMICO imetoa vifaa vya uchimbaji kwa Wachimbaji Wadogo viziwi ambao wameonesha nia ya kujishughulisha na uchimbaji.
Vifaa hivyo vimetolewa Novemba 26, 2021 katika kituo cha mfano kwa Wachimbaji Wadogo kilichopo Lwamgasa Mkoani Geita, kituo kinachoendeshwa na STAMICO.
Mara baada ya kukabidhi vifaa vya uchimbaji, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Wilson Shimo ameipongeza STAMICO kwa jitahada za kuwasaidia wachimbaji wadogo hususani kwa kuwakumbuka wachimbaji wa kundi hili maalumu.
“Naamini kwa vifaa hivi vitawasaidia kuongeza kasi katika uchimbaji na uzalisha wa Dhahabu. Nimeambiwa vifaa hivi vimegharimu zaidi ya Milion 10 hivyo tunataka kuona uchimbaji wenu unakuwa bora na wakisasa utakao wasaidia kwemye maisha yenu”, Mhe. Shimo
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Venance Mwasse amesema STAMICO imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuweza kuwashirikisha wachimbaji wadogo katika uchumi jumuishi kupitia shughuli zao wanazozifanya.
Amewapongeza wachimbaji hao kwa kuamua kujiishughulisha katika uchimbaji na kuachana na dhana potofu za kutumia ulemavu kama kinga ya kutokufanya kazi.
Amesema STAMICO itaendelea kuwa bega kwa bega na wachimbaji hao ili kuona wanaendelea kukua kwa kutumia Tekinolojia ya kisasa na kuchangia katika pato la Taifa.
Wachimbaji wadogo wenye usikivu hafifu msaada wa vifaa vya uchimbaji ambavyo vitawasaidia kwenye kazi zao. ” Sisi STAMICO tumeamua kuwasaidia nyavu wavue Samaki na sio kuwapa Samaki” Alisema Dr Mwasse.
Aidha, Mwenyekiti wa wachimbaji Wadogo Mkoa Geita Bw. Kadeo, ametoa rai kwa wachimbaji waliopatiwa vifaa, kutumia vyema vifaa hivyo kwa manufaa ili viweze kuleta tija kwenye shughuli zao za uchimbaji na akawasisitiza kutumia masoko ya madini yaliyopo kuuza dhahabu watakazozipata.
Kwa upande wa Wachimbaji Wadogo Mwenyekiti wa Taasisi ya Viziwi Tanzania (TAMAVITA) Bw.Nyema ameishukuru STAMICO kwa kusaidia na kuendelea kuwaamini wachimbaji hawa wenye usikivu hafifu na kuahidi kuvitumia vifaa hivi kwa umakili ili viweze kuwaletea manufaa.
STAMICO imeendelea kuwasaidia Wachimbaji Wadogo ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kupata dhahabu itayowasaidia kuwaletea maendeleo yao binafsi.