Home Uncategorized TWCC YAWAITA WAJASIRIAMALI MAONESHO YA 47 YA KIMATAIFA (SABASABA) JIJINI DAR 

TWCC YAWAITA WAJASIRIAMALI MAONESHO YA 47 YA KIMATAIFA (SABASABA) JIJINI DAR 

 Na: Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Mwajuma Hamza, amesema wataendelea kuwawezesha Wajasiriamali kushiriki katika maonesho ya Kimataifa ya 47 Sabasaba, ambayo yanatarajia kuaza Juni 28 hadi Julai 13, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Amesema maonesho ya Sabasaba yamekuwa chachu kubwa kwa washiriki wengi hususani kupata masoko ya uhakika wa Biashara zao nakwamba,  yatawakutanisha na wadau mbalimbali kutoka nje na ndani ya Tanzania.

Mwajuma ameyasema haya leo Mei 19,2023  katika mkutano na waandishi wa Habari ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) .ambapo amesema wao kama TWCC wanaendelea kuandikisha Wajasiriamali ili kushiriki kikamilifu maonesho hayo.

“Maonesho haya yamesaidia sana wajasiriamali wetu kupata masoko ya uhakika, hivyo ushiriki ni mkubwa na tunawaahidi Tantrade kuwa tutaendelea kuyatangaza maonesho haya ambayo yanatoa fursa ya watu kujitangaza na kuuza Biashara zao kwa viwango vya hali ya juu,” amesema.

Maonesho hayo ya Sabasaba ni ya 47 kufanyika tangu kuazisha kwake, na yamekuwa yakishirikisha Mataifa mbalimbali ambapo kwa mwaka huu tayari nchi 14 zimethibitisha kushiriki na zaidi ya makampuni 1000 ya ndani na nje ya Tanzania yamethiibitisha ushiriki wao.

Mwisho 

Previous articleNCHI 14 NA MAKAMPUNI  ZAIDI YA 1000 YATHIBITISHA KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA MWAKA HUU
Next articleMAONESHO YA SABASABA YANATOA FURSA KWA WAJASIRIAMALI KUJITANGAZA – AGATHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here