Home BUSINESS MAONESHO YA SABASABA YANATOA FURSA KWA WAJASIRIAMALI KUJITANGAZA – AGATHA

MAONESHO YA SABASABA YANATOA FURSA KWA WAJASIRIAMALI KUJITANGAZA – AGATHA

 DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Kampuni inayozalisha bidhaa zitokanazo na karanga ya Seasoning Palet Tobiproduct, Agatha Laizer amesema maonesho ya sabasaba yanatoa fursa kwao kama wajasiliamali kuweza Kujitangaza na kupata fursa kyonyesha kazi nzuri zinazofanywa na watanzania.

Pia Amesema kuwa maonyesho hayo ya kimataifa ya sabasaba ambayo yanafanyikia Kila mwaka hapa nchini yanawafanya wafanyabiashara kupiga hatua kwa kutumia majukwaa tofauti ambayo wanashiriki.

Agatha ameyasema haya leo Mei 19 mwaka huu katika viwanja vya maonyesho ya sabasaba vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo barabara ya kilwa wakati akizungumzia maandalizi ya maonyesho hayo ya sabasaba yanayotarajia kuaza Juni 28 na kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.

“Niwatie moyo wafanyabiashara wenzangu hasa wale wenye biashara ndogo ndogo katika maonyesho ya mwaka huu ya sabasaba tuyatimie vilivyo ili kuendelea kutengeneza matandao na Kujitangaza zaidi” amesema Agatha

Nakuongeza kuwa “tutakaposhiriki mwaka huu katika maonesho haya tutakuwa na uwezo wa kufanyakazi zaidi na kutengeneza mtandao mkubwa wa biashara ili kupata fursa mbalimbali zitakazotufanya tuzidi kuendelea mbele zaidi,” amesisitiza

Amesema anaishukuru TanTrade kwa kuanza maandalizi ya maonesho ya Sabasaba mapema hivyo amewataka wakinamama, vijana wasibaki nyuma kushiriki kwani anatambua kuwa wanabidhaa nzuri zenye ubora ambazo zinaweza kushindana na masoko mbalimbali ya nje ya nchi.

Ameongeza kuwa anawashukuru sana TanTrade Kwa kuweza kuwashirikisha katika maandalizi kwaniaba ya wajasiliamali wengine hivyo ni Imani yake kuwa wafanyabiashara na wajasiliamali wengi watapata fursa ya kushiriki kikamilifu kwenye maonyesho ya mwaka huu.

Pia Amesema kuwa Yeye kama mkurugenzi wa Kampuni ya palet Tobi product wamejipanga vizuri kwalengo la kuwaletea kitu kilicho Bora kupitia maonyesho ya kimaitafa ya sabasaba ambapo kwamujibu wa TanTrade kutakuwa washiriki wengi zaidi kutoka nje ya nchi na ndani ya Tanzania.

Mwisho .

Previous articleTWCC YAWAITA WAJASIRIAMALI MAONESHO YA 47 YA KIMATAIFA (SABASABA) JIJINI DAR 
Next articleRAIS MHE. DKT. SAMIA AZINDUA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU (AFRICA HEADS OF STATE HUMAN CAPITAL SUMMIT)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here