Na. Costantine James, Geita.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Geita imetoa elimu ya maswala ya kodi kwa walimu wakuu wa wahasibu zaidi ya 700 wa shule za msingi na sekondali katika halmashauri ya mji na wilaya ya Geita kwa lengo la kuwapa elimu ya kutosha juu ya maswala ya kodi.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita Adam Kobelo amesema wameamua kutoa elimu ya maswala ya kodi kwa walimu na wahasibu wa shule hizo ambayo itawawezesha kujua wajibu wao wa kisheria wakukata kodi ya zuio wakati wakufanya malipo katika shughuli mbalimbali zinazofanyika katika shule zao.
Walimu hao pia wamepatiwa elimu juu ya mfumo mpya wa kuwasilisha retun zao pamoja na kodi zinazohusiana na makato kwa njia ya mtandao amesema wameamua kuwapa elimu hiyo kutokana na serikali inapeleka fedha nyingi katika shule za msingi na sekondari na fedha hizo zinasimamiwa na walimu pamoja na wahasibu hao hivyo wanawajibu wakujua vizuri elimu juu ya kodi ya zuio ambayo itwasaidia kukusanya maoato ya serikali.
Akifungua semina hiyo Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe Ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya na Mkoa wa Geita kuendelea kutoa Elimu za mara kwa mara kwa Walimu pamoja na wahasibu wa shule za msingi na sekondari ili zinapoletwa fedha za miradi kwenye shule zao waweze kusimamia mapato ya serikali kwa usahihi zaidi.
Magembe amesema baadhi ya walimu wanakumbana na changamoto kubwa kutokana na kukosa elimu ya maswala ya kodi hasa serikali inapoleta fedha za kutekeleza miradi katika shule zao hivyo elimu hiyo itawasaidia pakubwa kukusanya mapato ya serikali wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo katika shule zao.
Nao baadhi ya walimu wakuu na wahasibu hao wameishukuru TRA mkoa wa Geita kwa kutoa elimu hiyo kwani awali walikuwa wanapata changamoto kubwa katika shughuli za malipo hasa ukataji wa kodi ya zuio kwenye shughuli za miradi shuleni kwao lakini sasa wamepatiwa elimu ya kutosha juu ya maswala ya kodi.