Home SPORTS TANZANIA YACHAPWA 1-0 NA UGANDA Canaf

TANZANIA YACHAPWA 1-0 NA UGANDA Canaf

Na: Stella Kessy,  DAR ES SALAAM

TIMU  ya Uganda  leo imeibuka na ushindi dhidi ya  Tanzania kwa bao 1-0 katika  mashindano yanayoendelea  ya Afrika  soka  kwa wenye ulemavu CANAF 2021 katika  Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika dakika 20 mshambuliaji Ssempija Julius wa Uganda  aliipatia timu yake bao ambalo lilidumu dakika zote za mchezo.

Katika mchezo wa kwanza Tanzania iliibamiza timu ya Morocco 2-1. Wakati Uganda katika mchezo wake na Sierra Leone walifungwa 3-0.

Mchezo huu umechezeshwa na  Luciano Antonio kutoka Angola, Mohamed Mwadini kutoka Zanzibar na David Mng’ong’o kutoka Tanzania.

Mechi nyingine kati ya  Morroco imeibuka na ushindi wa bao 3-0 

Huku  bao yote yamefungwa na Redouane Chaanoun  huku mchezo mwingine ukiwa kati ya Kenya na Zanzibar, Liberia na Gambia pia Nigeria na Misri.

Previous articleMIAKA 60 YA UHURU IDARA YA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA JIJI WAFANYA USAFI
Next articlePABLO AKOSHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here