Home BUSINESS SERIKALI KUSHIRIKISHA WANANCHI KUHUSU KUONDOLEWA KWA KIJIJI CHA NGARESERO KWENYE PORI TENGEFU...

SERIKALI KUSHIRIKISHA WANANCHI KUHUSU KUONDOLEWA KWA KIJIJI CHA NGARESERO KWENYE PORI TENGEFU LA POLOLET, NGORONGORO

Serikali imesema kuwa itashirikisha wananchi kuhusu utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri ya kukiondoa Kijiji cha Ngaresero katika Pori Tengefu la Ziwa Natron kutokana na sababu kwamba Pori hilo ni moja kati ya maeneo yaliyotolewa maelekezo na Baraza la Mawaziri kuwa lipandishwe hadhi.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Mhe. Emmanuel Lekishon Shangai, lililoulizwa na Mhe. Zaytun Swai kuhusu lini Serikali itaondoa Kijiji cha Ngaresero kwenye eneo la Pori Tengefu la Pololet baada ya kujumuishwa kimakosa.

Amefafanua kuwa kulingana na Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na marekebisho yake ya mwaka 2019, ardhi ya Pori Tengefu Ziwa Natron ipo kwenye kundi la ardhi ya Hifadhi.

Aidha, Mhe.Masanja ameweka bayana kuwa Serikali itaenda kushughulikia mgogoro huo kwa kukutana na wananchi ili kufikia muafaka na hatimaye pori hilo liwe na hadhi iliyotarajiwa.

Previous articleDART YAJIPANGA KUTENGENEZA MIUNDOMBINU YA BARABARA MIKOA INAYOKUWA KWA KASI
Next articleTMDA YATOLEA UFAFANUZI KUHUSU UVUMI WA DAWA AINA YA P-500 (PARACETAMOL)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here