Home SPORTS MASHINDANO YA MPIRA WA MIKONO AFRIKA YASHIKA KASI DAR

MASHINDANO YA MPIRA WA MIKONO AFRIKA YASHIKA KASI DAR




Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MASHINDANO  ya  Mpira wa Mikono Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati yanaendelea kushika kasi kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa ,Dar Es Salaam.

Matokeo yamechi za jana  maafande  wa JKT Wanawake na Wanaume wameanza vibaya,JKT wanaume walikubali kichapo cha magoli 

42-19 dhidi ya Selieols kutoka Kenya ,huku upande wa Wanawake wakipoteza kwa magoli 43_19 dhidi ya Nairobi water katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa kwenye uwanja huo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mikono Tanzania(  TAHA) Michael Chibawala,amesema kuwa mashindano hayo yameshirikisha Klabu 11 kutoka nchi ya Kenya ,Rwanda na Tanzania wenyeji.

Amesema kuwa lengo ni kupata Klabu nne za juu,mbili Wanawake na mbili wanaume watakaofuzu kushiriki mashindano ya Vilabu Afrika yatakayofanyika mwakani.

“Maandalizi yapo vizuri lakini tuliratajia kuwa na Klabu 19  kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zingine zimeshindwa kufika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo,hivyo kwa walioshiriki tunatarajia kuona ushindani na kutimiza malengo tuliokusudia,” alisema Chibawala.

Alitaja klabu nyingine shiriki ni ya wanaume  Black Mamba(Kenya)Polisi Rwanda, Ngome (Tanzania), na Nyuki  (Zanzibar),  huku wanawake Kizugiro(Rwanda)  na  Ngome(Tanzania).

Naye Katibu Mkuu wa TAHA Nicholous Mihayo,alisema kuwa alisema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha mchezo wa Mikono unaendelea  na kuwa juu zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt Hassan  Abbas,aliwashukuru waandaaji  kufanikisha kuandaa mashindano hayo.

Mbali na hao pongezi zilienda kwa timu shiriki  na kuzitaka kila la heri ya mashindano hayo.





.

Previous articleMAMILIONI YA WATU WAISHIO VIJIJINI WANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA SBL KWENYE MAJI SAFI NA SALAMA
Next articleTANZANIA YATINGA ROBO FAINALI Canaf
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here