Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa Wenye Ulemavu (Tembo Warriors), imezidi kufanya vyema katika michuano kwa kuipa hadhi nchi kuwa Taifa la kwanza Afrika, kufuzu kwenda Robo Fainali za Mashindano ya Soka kwa Walemavu Afrika (Canaf), ambayo Tanzania ni mwenyeji.
Tanzania imepata nafasi hiyo baada ya leo kuifunga timu ngumu ya Taifa ya Sierra Leone bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Huku bao pekee la Tanzania limefungwa na Frank Ngairo bao katika dakika za 31 ambalo limedumu katika dakika zote za mchezo.
Akizungumza na wachezaji baada ya mechi kuisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa ni jambo la furaha kwa Tanzania.
“Sasa tuna mechi moja mbele kabla ya kupata tiketi mbili muhimu; moja ni kuingia nusu fainali lakini tukishinda mechi hiyo moja pia tutakuwa tumefuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani mjini Instanbul, Uturuki,”
Timu ambayo imetinga katika hatua ya robo fainali ni morroco kwa kuichapa Uganda bao 3-1
Amesema kuwa lengo ni kupata Klabu nne za juu,mbili Wanawake na mbili wanaume watakaofuzu kushiriki mashindano ya Vilabu Afrika yatakayofanyika mwakani.
“Maandalizi yapo vizuri lakini tuliratajia kuwa na Klabu 19 kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zingine zimeshindwa kufika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo,hivyo kwa walioshiriki tunatarajia kuona ushindani na kutimiza malengo tuliokusudia,” alisema Chibawala.
Alitaja klabu nyingine shiriki ni ya wanaume Black Mamba(Kenya)Polisi Rwanda, Ngome (Tanzania), na Nyuki (Zanzibar), huku wanawake Kizugiro(Rwanda) na Ngome(Tanzania).
Naye Katibu Mkuu wa TAHA Nicholous Mihayo,alisema kuwa alisema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha mchezo wa Mikono unaendelea na kuwa juu zaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas,aliwashukuru waandaaji kufanikisha kuandaa mashindano hayo.
Mbali na hao pongezi zilienda kwa timu shiriki na kuzitaka kila la heri ya mashindano hayo.