Home LOCAL NAMTUMBO WATAKIWA KUONGEZA KASI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

NAMTUMBO WATAKIWA KUONGEZA KASI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

 Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu akimueleza jana Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge juu ya kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inavyoendelea wilayani humo wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa chini ya fedha za mpango  wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid 19.


Mkuu wa shule ya Sekondari Nanungu wilaya ya Namtumbo Judith Ndomba katikati,akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge aliyetembea shulu hiyo kuangalia kazi ya ujenzi wa madarasa inavyoendelea,wa pili kulia Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu na kulia Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiangalia ubora wa viti na meza katika shule ya sekondari Nasuli wilaya ya Namtumbo vinavyotengenezwa kwa ajili ya  kutumia wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza muhula wa masomo 2022.


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,akiongea na wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari Nasuli wilayani humo ambapo aliwataka kusoma kwa bidii na kuzingatia yale wanaoyfundishwa na walimu wao ili waweze kutumiza ndoto zao.


Mkuu wa shule ya sekondari Nasuli wilayani Namtumbo Dafrosa Chilumba kulia,akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge vinavyojengwa katika shule hiyo kupia mpango wa maendeleo na usatwi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid 19,katikati Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Julius Ningu.


Mbunge wa Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma Vita Kawawa akimueleza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigendia Jenerali Wilbert Ibuge changamoto iliyosababisha baadhi ya vyumba vya madarasa katika wilaya ya Namtumbo kusua sua ambapo alisema, hali hiyo imetokana na tatizo la upatikanaji wa vifaa vya ujenzi ,kulia Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Julius Ningu.

Picha zote na Muhidin Amri,

Na: Muhidin Amri, Namtumbo

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,amewaagiza viongozi wa wilaya ya Namtumbo kuongeza kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na miundombinu mingine ya elimu kukamilika kabla ya Tarehe 10 Mwezi Desemba mwaka huu.

Ibuge ametoa agizo hilo jana, wakati akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kupitia mpango wa maendeleo wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid 19 wilayani humo.

Mkuu wa mkoa alisema,hajaridhishwa na  na kasi ya utekelezaji wa miradi ya Covid -19 katika wilaya hiyo kwa kuwa,bado ujenzi wake  unakwenda kwa kusua sua  ikilinganisha na miradi inayojengwa kwenye  wilaya nyingine, ambapo ametoa wiki mbili  wawe wamekamilisha kazi hiyo.

“maeneo mengine nimekuta mafundi zaidi ya mmoja katika  darasa ,kuna wanaopiga lipu,kufunga milango,madirisha, na kupaua lakini katika miradi yenu hapa mafundi ni wachache,kwa hiyo naagiza miradi yote iwe imekamilike kabla ya tarehe 10 Desemba” alisema Ibuge.

Aidha amewataka viongozi wa wilaya hiyo, kuhakikisha vifaa vinavyotumika katika ujenzi huo vinakuwa na ubora unaotakiwa ili kuwezesha kupata madarasa bora na viwango vya hali ya juu badala ya kujenga kwa kubabaisha.

Ibuge,ametaka kila mmoja kusimamia miradi hiyo kwenye eneo lake ili wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari mwezi Januari mwakani wapate nafasi kwenye shule watakazopangiwa.

Jenerali Ibuge alisema,Serikali imetoa fedha nyingi za miradi  kwa Halmashauri hiyo zikiwemo za utekelezaji wa miradi ya Covid-19 na  lengo ni kuhakikisha miundombinu ya elimu ina kuwa bora na wanafunzi wanapata fursa ya kusoma na kufanya vizuri kwenye masomo.

Katika ziara hiyo ambayo alifuatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, alitembelea shule ya sekondari Nanungu,Mtakanini,Msindo, Nasuli na Narwi ambazo ujenzi wake uko katika hatua mbalimbali.

Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa, ameishukuru serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta ya elimu na afya ambayo itaongeza morali ya wanafunzi kusoma kwa bidii.

Hata hivyo alisema, changamoto kubwa ni kuchelewa kwa ujenzi wa miradi hiyo kutokana na upatikanaji wa vifaa kutoka kwa wafanya biashara waliopandisha bei ya vifaa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Julius Ningu alisema,watafanyia kazi maelekezo ya Mkuu wa mkoa na kuhaidi ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa  vitakamilika kwa muda uliopangwa.

Mkuu wa shule ya sekondari Mtakanini Michael Kabogo alisema, wamepokea jumla ya Sh.milioni 40 kwa ajili ya kujenga vyumba viwili vya madarasa na hadi sasa fedha zilizotumika ni Sh. 12,937,700 na salio Sh.27,062,300.
MWISHO.

 

Previous articleMADARASA 332 KUKAMILIKA IFIKAPO DESEMBA –RC MKIRIKITI
Next articleREA YAVUKA MALENGO KUWAFIKIA WANANCHI VIJIJINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here