Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Mohamed Mchengerwa akifungua semina ya viongozi wa Tughe mahala pa kazi.
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Mohamed Mchengerwa amewaagiza waajiri wote nchini kuchukua hatua kuwaondoa katika nafasi zao baadhi ya maafisa watumishi walioshiriki kuficha madalaja ya watumishi ili kuzuia wasipandishwe vyeo.
Mchengerwa aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa Tughe mahala pa kazi na waajiri yaliyofanyikia jijini Arusha ambapo aliwataka waajiri kwenda kuwashusha vyeo maafisa utumishi hao na nafasi hizo wawekwe watu wenye uwezo ambao watakuwa tayari kusikiliza kero za watumishi wenzio na watakao kuwa tayari kujitoa katika nchi yao.
“Mkawatoe na kuwaweka watu watakaokuwa tayari kuwatumikia watumishi wa umma, na ninaposema waondolewe namanisha ili tupate watu walio tayari kutumika nchi na sio matumbi yao na hii itasaidia kila kiongizi katika eneo lake kutengeneza mazingira yatakayoleta mapinduzi ya kifikra,”Alisema Mchengerwa.
Alifafanua kuwa ni lazima kila mmoja akabadilisha mitazamo yake kwasababu serikali ya sasa haitaki uonevu na Kuna watumishi ambao hawapendi kuona wenzao wanafanikiwa na wakipewa nafasi wanadhani miji yote ni ya kwao bila kufahamu kuwa vyeo hivi ni vya kupita na utumishi wa umma una muda.
“Nataka niwaambie sekta ya utumishi tutapiga hatua kwasababu Rais tuliyenae ni msikivu na ni Rais anauetenda haki hivyo maafisa utumishi acheni tabia ya kuficha majalada ya watumishi wenzenu haipendezi na sio vizuri na nakuja na mkakati wa kupambana na jambo hili moja kwa moja na kwa kuanza nitahitaji kazi data ya watumishi wote ili niweze kujua flani ni nani, kazi yake ni ipi na ana kiwango gani cha elimu,” Alisema.
Naye katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi Tughe taifa Herry Mkunda alisema mafunzo hayo yanalenga kuleta uelewa wa pamoja katika masuala ya waajiri na watumishi lakini pamoja na ushirikiano huo bado wanakabiliwa na changamoto ya uwepo wa baadhi ya vifungu vya sheria na kanuni ambazo zinaweza kuleta mgongano katika utendaji kazi.
“Mfano kifungu cha 32 cha sheria ya utumishi wa umma sura namba 298 inatoa fursa kwa watumishi waliokatika ajira za kawaida sura namba 396 kutumia sheria ya mahusiano kazini marejeo ya 2019 ikiwa vifungu hivi vinapingana na kifungu za 32a cha sheria hiyohiyo,”alisema Katibu huyo.
Mkunda alisema vifungu hivyo vinapingana na kifungu 32a cha sheria ambacho kinazuia watumishi wote wa umma wasitumie utaratibu wa sheria ya ajira ya mahusiano kazini kwani umekuwa ukiwapa tabu pale wanapopata changamoto mashauri ya kiutumishi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tughe Taifa, Joel Kamnyonge alisema ni vyema waajiriwa wa serikali waliyoko kwenye hospitali teule wakakumbukwa kwani wamesahauliwa kwa kutojulikana pamoja na kupata mishahara lakini wametelekezwa ikiwa wengi wao wamepoteza haki ya kupandishwa vyeo kwa muda mrefu.
“Idara ya wauguzi haki zao zimesahulika kidogo ni vyema waziri mwenye dhamana ukaangalia suala hilo kwa undani zaid lakini Pia maafisa ugani wa kilimo na mifugo hawaonekani kwani wanaonekana kama wanafanya kazi Malawi hivyo tunaomba pia serikali kupitia wizara yako kuangalia kazi hiyo iendane na utumishi huu kwa nafasi walizonazo,”alisema Mwenyekiti huyo.