Zifuatazo ni sababu za rangi nyekundu kuwa chaguo la timu mbalimbali duniani.
Moja ya sababu za timu za soka kuchagua kuvaa jezi nyekundu ni utamaduni. Kwa mfano, Manchester United wana historia ndefu ya kuvaa jezi nyekundu tangu miaka ya 1902. Rangi nyekundu imekuwa sehemu ya utambulisho wa klabu hiyo na hata kujipatia jina la Red Devils kwa maana ya Mashetani Wekundu.
Sababu nyingine ya kuvaa jezi nyekundu ni muonekano. Rangi nyekundu ni rangi nzito na inayong’aa ambayo inaweza kuonekana vizuri uwanjani. Hii inasaidia watazamaji kuona wachezaji wa timu zao pendwa hata kama wamekaa viti vya juu au viti vilivyo mbali.
Rangi nyekundu pia ina ashiria nguvu. Kila timu inataka kuonekana ina uwezo kuliko mpinzani wake. Hivyo, rangi saa nyingine inatumika kama lugha ya utambulisho kwenye sekta ya kupimana. Mfano, kuna wale wa Liverpool na kwa Tanzania kuna timu ya Simba. Kwa lugha ya mtaani tunasema timu gani imekaa kibabe zaidi?!
Utambulisho wa Taifa. Timu za taifa kama Morocco, Ureno na Vietnam hutumia rangi nyekundu katika mavazi yao ya jezi. Hii yote ni kutokana na rangi nyekundu kuwa rangi husika ya bendera za mataifa yao. Hili ni kama jambo la kizalendo kujivunia taifa na kuliwakilisha kwa rangi husika katika michezo ya kimataifa.
Kwa kuhitimisha, kuchagua rangi ya jezi ya soka kunaweza kuwa uamuzi mgumu, lakini uwepo wa rangi nyekundu imerahisisha mambo maana ni rangi moja inayonekana sana, imekaa kibabe na inavutia pia. Rangi hii inachangia kunogesha lugha ya utani haswa kwa wale wanaopenda sports betting Mfano, mtu akitweet “MASHETANI WEKUNDU WAMEWAKA!” anahamasisha kuliko yule anaeandika “MANCHESTER UNITED WAMEWAKA.”
Na huo ndo utofauti wa kutumia rangi nyekundu kwenye jersey za timu mbalimbali.