Home LOCAL KINANA: VIJANA, WANAWAKE JITOKEZENI UCHAGUZI NDANI YA CCM TUTATENDA HAKI

KINANA: VIJANA, WANAWAKE JITOKEZENI UCHAGUZI NDANI YA CCM TUTATENDA HAKI

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka akiwa katika matembezi na viongozi wa CCM na Serikali Mkoa wa Katavi alipokuwa akikagua ujenzi wa fremu 118 zilizopo Mpanda mjini mkoani Katavi.

Na:Said Mwishehe, Michuzi TV

MAKAMU Mwenyezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amewahimiza Wananchi hasa wanawake na vijana kujitokeza na kuchukua fomu kuwania nafasi za uongozi wa ndani ya Chama hicho na watakaochukua fomu haki itatendeka na hakuna wa kumtisha mwenzake.


Akizungumza leo Julai 25,2022 baada ya kuzindua Mradi wa fremu za maduka 15 zilizojengwa kwenye eneo la Ofisi za CCM Mkoa wa Katavi,Kinana pamoja na mambo na mengine ameelezea mchakato wa uchgauzi wa ndani wa Chama hicho unavyoendelea ambapo amewahimiza wanawake na vijana kuchukua fomu kigombea nafasi za uongozi.


“Niwaombe akina mama mkachukie fomu za kuwania nafasi za uongozi CCM, msiogope nendeni mkachue fomu mpambane na wanaume.Pia nataka niwasihi vijana gombeeni hizo nafasi, Uchaguzi ukija nafasi zitakuwa wazi na kila mtu anahaki sawa na mwenzake.

“Hakuna masultani wa kukaa madarakani milele,tuna uchaguzi kila baada ya miaka mitano, wenye kuwachagua Wana CCM ,wana CCM wakikupenda ,wakikuheshimu na wakithamini mchango wako watakupa kura lakini wasipothamini watakunyima kura.

“Nafikiri na ninyi mnawafahamu wajumbe sio watu wazuri ,wajumbe hao wanaweza kukwambia usiwe na wasiwasi tutakupa kura, halafu baadae unatoka kapa, hivyo niwaombe sana vijana gombeeni ,kina mama gombeeni,tutatenda haki,hatutampendelea mtu.

“Wala mtu asimtishe mwenzake kwamba ukienda kuchukua fomu unaambiwa na wewe unatafuta nini,kwani na wewe ulivyochukua si mwingine alikuwepo kabla yako, ndio umechukua nafasi yake na mimi nakuja kukung’oa wewe,”amesema Kinana.

Wakati Kinana akiyaeleza hayo Wana CCM na wananchi waliokuwa eneo hilo la Ofisi za CCM Mkoa walionekana kufurahia kwa kupiga makofi na vigele.Kwa kukumbusha tu Chama hicho kwa sasa kinaendelea na Uchaguzi wake wa ndani na wanaCCM wameendelea kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali.


Awali akipokea taarifa kuhusu ujenzi wa fremu hozo Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi Omari Mtuwa amesema ujenzi wa fremu hizo umegharimu Sh.milioni 65 na waliokodisha fremu hizo kwa mwezi watakuwa wanalipa Kodi Sh.100,000.”Tumeingia mkataba na waliojenga fremu hizi na leo tunafurahi Makamu wa CCM Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana umezindua.


Kinana ambaye ameongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka amewasili mkoani Katavi leo na akiwa katika Mkoa huo pamoja na mambo mengine amekaguaa miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.



Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Katavi baada ya kuwasili katika wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi kwa ajili ya kukagua na kuweka jiwe la Msingi kituo cha Afya cha Itenka.PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI.



Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akichota udongo kuweka kwenye mti alioupanda nje ya Ofisi za CCM Mkoa wa Katavi ikiwa ni ishara ya kufika kwake katika ofisi hizo baada ya kuzindua mradi wa fremu 15 za maduka ya biashara.Wengine wanaoshuhudia ni viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama na Serikali katika mkoa huo.

Baadhi ya Wanachama wa CCM na Wananchi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akizindua fremu 15 za maduka yaliyojengwa katika majengo ya Ofisi za CCM mjini MPanda mkoani Katavi

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi mradi wa fremu 15 za maduka ya biashara zilizojengwa katika eneo la ofisi za CCM,Mpanda Mkoani Katavi.Kinana amezindua mradi huo leo Julai 25,2022 baada ya kuwasili mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi sambamba na kukagua miradi ya maendeleo.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa fremu 15 za maduka ya biashara yaliyojengwa katika Ofisi za CCM Mpanda mjini Mkoa wa Katavi.Wengine wanaoshuhudia ni viongozi wa Chama na Serikali mkoa huo pamoja na wananchi


Previous articleTAMISEMI YATOA ONYO KUHUSU MIUNDOMBINU, HUDUMA ZA AFYA KILWA
Next articleWAZIRI NDALICHAKO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here