Home LOCAL RC SENYAMULE AKAGUA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA GEITA

RC SENYAMULE AKAGUA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA GEITA

Na: Paul Zahoro, Afisa Habari, Geita RS.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule leo tarehe 02 Disemba, 2021 amefanya ziara wilayani Geita kukagua miradi ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa yanayojengwa na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19.

Akikagua ujenzi kwenye Shule ya Sekaondari Nyarugusu wanaojenga vyumba 8 vya Madarasa kwa Tshs. Milioni 160 Mhe. Mkuu wa Mkoa amehimiza uharakishwaji wa ujenzi na ameitaka  kamati ya ujenzi ya shule hiyo kutekeleza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.

“Ni lazima tuunganishe nguvu za viongozi na wananchi kwa kushirikiana hivyo basi waelewesheni wananchi kuwa wakisaidia ujenzi nguvu zao zitaweka alama kwenye shule zao wenyewe, naomba tuongezeni hamasa kwenye ujenzi huu.” Amesema Mkuu wa Mkoa.

“Kasi ya uhitaji wa mawe, mafofali na mchanga kwa sasa sio sawa na ile ya siku za nyuma, mahitaji sasa hivi ni makubwa sana lazima tuwe wabunifu kwenye kutekeleza ujenzi huu.” Mhe. Wilson Shimo, Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Mhe. Swalehe Juma, Diwani wa Kata ya Nyarugusu amesema sababu za kijiografia zimesababisha pia ugumu kwenye ujenzi wa Vyumba vya madarasa kama miinuko iliyopo kwenye shule hiyo kupelekea mahitaji ya udongo kuwa zaidi ya makisio ili kujaza kwenye madarasa.

“Mradi umepata Changamoto za kutopata vifaa kwa wakati, bei ya vifaa kuwa juu tofauti na kwenye maelekezo kama Tripu ya Mawe kuuzwa laki 1 badala ya Elfu 70 iliyobajetiwa, Mbao kuuzwa ghali, Madirisha na Vigae vya ujenzi kwa wakati japo madarasa yote 8 yatakamilika hadi kufikia disemba 15 pamoja na samani.” Amesema Mkuu wa shule ya Sekondari Nyarugusu.

“Walipeni wazabuni ili kazi ifanyike kwa spidi kubwa, wazabuni wanagombaniwa hivyo wanatoa huduma pale kwenye matumaini ya kuwa kuna pesa sio maneno tu.” Amesisitiza Mhe. Mkuu wa Mkoa wakati akikagua ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa kwenye Shule ya Sekondari Evaristi.

“Dhamira yashinda vikwazo, ukiwa na nia na jambo hata kukitokea changamoto utajitahidi kuzitafutia ufumbuzi ili kuhakikisha unamaliza tatizo hilo hiyo ndio hali ya binadamu anayetafuta majibu ya jambo fulani.” Mkuu wa Mkoa kwenye shule ya Sekondari Busanda.

“Magenge  Sekondari wamepata Milioni 120 kujenga madarasa 6 kwa ushirikiano Mkubwa wa Mhe. Diwani na Mtendaji tuliweza kujikopa na mkakati wetu ni kwamba kufikia tarehe 05 tutafikia hatua kubwa sana,” Amesema Mkuu wa Shule.




Baadae Mhe. Mkuu wa Mkoa alifika kwenye shule ya Sekondari Kaseme wanaojenga vyumba 8 vya Madarasa kwa Jumla ya Tshs. Milioni 160 ambapo amebaini ucheleweshaji wa vifaaa na kisababisha kuchelewa kutekeleza mradi huo na kuwa kwenye hatua ya linta hadi sasa.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake ya kuangazia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha dhamira ya kuwapatia wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia kwenye Shule za Sekondari Nyankongochoro na Lubanga ambao wanajenga madaraasa 10 kwenye kila shule kwa Tshs. Milioni 200 (Milioni 400) na amewataka kuongeza ubunifu kwenye utatuzi wa changamoto ili wakamilishe kwa wakati.
Previous articleWATAKIWA KUTUMIA KAMPUNI ZILIZOSAJILIWA BRELA
Next articleUTEUZI:RAIS SAMIA AMTEUA BALOZI SALOME SIJAONA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA ARDHI (ARU)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here