Home SPORTS TANZANIA YAKAMATA TANI 356 ZA DAWA ZA KULEVYA

TANZANIA YAKAMATA TANI 356 ZA DAWA ZA KULEVYA

Na: Ahmed Sagaff – MAELEZO

Serikali ya Tanzania imekamata tani 356 za dawa za kulevya kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Gerald Kusaya alipozungumza na wanahabari kuhusu mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.

“Mamlaka toka kuanzishwa kwake mwaka 2017 hadi kifikia mwishoni mwa Septemba 2021 kwa kishirikiana na vuombo vingine vya dola ilifanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 45,784 wa dawa za kulevya, kilogramu 356,563.1 za dawa za kulevya pamoja na kuteketeza ekari 628.75 za mashamba ya bangi,” alieleza.

Akitoa ufafanuzi, Bw. Kusaya ameitaja bangi kuongoza katika orodha ya dawa za kulevya zilizokamatwa.

“Dawa za kulevya zilizokamatwa ni kilogramu 1,125.41 za heroin, kilogramu 26.67 za cocaine, kilogramu 199,740 za bangi, kilogramu 97,640 za mirungi, kilogramu 57,600 za kemikali bashirifu na kilo 431.02 za methamphetamine,” amearifu.

Previous articleALIYOYASEMA KAMISHNA JENERALI DCEA GERALD KUSAYA WAKATI AKIELEZA MAFANIKIO YA MAMLAKA HIYO MIAKA 60 YA UHURU
Next articleGHANA, LIBERIA KUUMANA FAINALI ZA CANAF KESHO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here