Home BUSINESS SERIKALI YA RAIS SAMIA IMEJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA: DKT. HASHIL

SERIKALI YA RAIS SAMIA IMEJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA: DKT. HASHIL


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Maonyesho ya Bidhaa za Usafirishaji kutoka India, Disemba 2, 2021, Diamond Jubilee, Dar es salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akikagua Bajaji wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Bidhaa za Usafirishaji kutoka India, Disemba 2, 2021, Diamond Jubilee, Dar es salaam



DAR ES SALAAM.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil  Abdalah amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuimarisha sekta ya viwanda na biashara kwa kuhakikisha wafanyabiashara wananufaika na Serikali inanufaika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo  alipokuwa akifungua maonyesho ya bidhaa za usafirishaji ambazo zinaingizwa nchini kutoka  India katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Disemba 2, 2021 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari, wafanyabiashara na wananchi waliofika katika maonyesho hayo Dr. Abdallah amesema Maonyesho hayo ni muhimu  katika kukiza uchumi wa  nchi  kwa kuwa vifaa vya usafirishaji kama Pikipiki, Bajaji, Matrekta magari  vinatumiwa na wananchi wengi katika kurahisisha shughuri zao za kila siku.

“Bidhaa hizi mfano Matrekta, Bajaji, Pikipiki zinaingia sokoni kama mitaji ambayo inatumika na watu kujiendeleza kiuchumi ” Amesema  Dkt. Absallah.

Aidha, Dkt. Abdallah amesema Wizara ya Viwanda na Biashara ipo tayari kutoa  ushirikiano na kutatua changamoto ambazo zinawakabili wafanya biasharawakati wowote  kwa kushirikiana na wadau wengine.

Naye,  Balozi wa India  nchini Tanzania, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amesema ingawa kwa sasa bidhaa hizi zinazalishwa nchini India, hivi karibuni zitaanza kuzalishwa nchini Tanzania.

Dkt. Abdallah ametoa rai kwa watanzania kufika katika maonyesho hayo kuzungumza moja kwa moja na wafanyabiashara na benki zilizopo hapo ili kuona namna ya kutumia fursa hii kujinufaisha.

Previous articleGHANA, LIBERIA KUUMANA FAINALI ZA CANAF KESHO
Next articleRAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA RADDY FIBER MANUFACTURING LTD,MKURANGA PWANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here