Musoma.
MKUU wa Wilaya ya Musoma, Dkt Khalifan Haule, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Msongela Palela na Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo wanatarajiwa kuongoza Uzinduzi wa Kampeni ya Sensa ya Watu na Makazi, itakayofanyika jimboni humo, Jumamosi, 30 Julai 2022.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Leo, Julai 26 Julai 2022 na Ofisi ya prof. Muhongo,
Kampeni hiyo itafanywa ndani ya Kata zote 21 za Jimbo hilo zenye Vijiji 68.
Imeelezwa kuwa uzinduzi huo utaanza Saa 9:00 Alasiri kijijini Busekera na kwamba kampeni itaendelea hadi 22 Agost Mwaka huu, kabla ya sensa kuanza 23 Agosti 2022.
“Vikundi vya Uhamasishaji ambavyo vimetayarishwa na Mbunge wa Jimbo (Prof. Muhongo vitakuwa vikitumbuiza katika kampeni hiyo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Vimetajwa kuwa ni pamoja na Kwaya ya Bugoji, Kwaya ya Kiriba, Ngoma ya Liranda Bugwema, Ngoma ya Kiwanjuki Kiriba, Ngoma ya Mbegete Nyakatende na Mtelezo Show ya Nyakatende.
Sanjali na hayo, kimetengenezwa Kipepeeushi chenye kurasa Mbili ambacho kinagawiwa kwa wakazi wa Vijiji vyote 68, kikitoa elimu sahihi kuhusu masuala yote muhimu na ya msingi juu ya Sensa hiyo.