Home LOCAL WATAKIWA KUONGEZA KASI YA KUPIMA ARDHI

WATAKIWA KUONGEZA KASI YA KUPIMA ARDHI

Picha Na: Maktaba

Na: Lucas Raphael, Urambo

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza halmashauri ya wilaya ya urambo mkoani Tabora kuongeza kasi ya kupima na kumilikisha viwanja ili kutatua migogoro ya ardhi

Alitoa Agizo hilo jana kwa viongozi wa wilaya ya urambo wakati wa ziara ya siku moja wilayani humo na kusisitiza kwamba lengo ni kuwawezesha wananchi katika sekta ya ardhi

Dkt Angeline Mabula Alisema umilikishaji wa maeneo yao huwa kichocheo cha shughuli za maendeleo ikiwemo kupata mikopo benki kuweka dhamana na kupunguza migororo ya ardhi

Sambamba na Agizo hilo Naibu waziri aliipongeza halmashauri ya wilaya ya urambo kwa kufanya kazi kwa malengo yaliyolengwa na wizara licha kuwa na uhaba wa watumishi na kuwaitaka halmashauri hiyo kuitumia ofisi ya ardhi ya mkoa ili kuwasaidia katika utendaji kazi

Awali afisa ardhi wa wilaya ya urambo Joel Mapunda alisema walikuwa wakikwamishwa na uhaba wa vitendea kazi jambo ambalo limeshatafutiwa ufumbuzi na kwa sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya urambo Louis Bura aliishukuru wizara kwa kuutatua mgogoro uliokuwepo kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi na kuongeza kuwa maagizo yake wameyapokea na wataenda kuyafanyia kazi.

Halmashauri ya wilaya ya urambo imepima na kugawa hati ya viwanja 106 kati ya viwanja 865 katika kata ya urambo .

mwisho

Previous articleMAKAMU WA RAIS AFUNGUA KIKAO NCHI WANACHAMA WA AU
Next articleSTAMICO YATANGAZA BIDHAA MPYA YA MKAA MBADALA (RAFIKI BRIQUETTES) ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here