Home LOCAL WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA BARAZA LA KUTOKOMEZA MALARIA NCHINI

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA BARAZA LA KUTOKOMEZA MALARIA NCHINI

Na: WAF – Dar Es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua rasmi Barala la Taifa la Kutokomeza Malaria nchini ambalo litasaidia kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali kutoka katika vyanzo vya ndani ambavyo vitawezesha kupunguza pengo la uhitaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza afua za udhibiti wa Malaria.

Halfa ya uzinduzi wa Baraza hilo imefanyika leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo Kitaifa yameadhimishwa Jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Baraza hili lenye wajumbe 19 ili kuongeza hamasa zaidi za mapambano dhidi ya malaria na kusaidia kwenye ukusanyaji wa rasimali mbalimbali kwa ajili ya mapambano hayo na kufanikiwa kuutokomeza ifikapo mwaka 2030” amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Leodigar Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo ambalo limesheheni watu mashuruhi wenye ushawishi ndani ya jamii wakiwemo, Mfanyabiasha maarufu Said Salim Bakhresa, Wasanii Naseeb Abdoul (Diamond Platmunz), Zena Mohammed (Shilole) Viongozi wa Dini wakiwemo Askofu Fredrick Shoo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abooubakar Zuberi pamoja na wajumbe wengine kutoka taasisi za fedha na asasi za kijamii.

Waziri Mkuu ameelekeza kuwa rasilimali ambazo zitakusanywa na Baraza hilo zitumike vizuri kwenye utekelezaji wa afua za mapambano dhidi ya Malaria kwa ushirikiano kutoka Wizara ya Afya.

Waziri Mkuu ameelekeza Baraza hilo kuandaa Mpango kazi wa utekelezaji wa shughuli zake mapema, pamoja na kuainisha mahitaji na maeneo kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa majukumu yao.

“Baraza hili litachangia sana katika kupunguza pengo la upatikanaji wa rasilimali na kuleta tija katika mapambano dhidi ya malaria na tunaamiji kwa mchanganyiko wa wajumbe waliopo tutapata mafanikio makubwa sana” amesema Waziri Mkuu

Awali akizungumza, Waziri wa Afya Mhe. Ummy amesema uanzishwaji wa baraza hilo ni sehemu ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa rasilimali za kutekeleza baadhi ya afua za Malaria.

“Uundwaji wa Baraza hili unatokana na maazimio ya Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwenye mikutano yao ya mwaka 2016 na 2017, ambapo kwa pamoja waliazimia kuimarisha mikakati ya kudhibiti Malaria ili kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030 ikiwemo uhamasishaji wa upatikanaji wa rasilimali za kutekeleza mikakati hiyo kwa kuunda Mabaraza ya Kutokomeza Malaria.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Amesema wajumbe wengine wanaoingia kwenye Baraza hilo kuwa ni Waziri wa Afya kwa nafasi yake, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na watendaji wakuu wa Wizara hiyo ikiwemo Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Previous articleTANZANIA YAPIGA HATUA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA
Next articleTANZANIA KUFANYA MAONESHO YA SABA YA UTALII, (SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO-S!TE), MWEZI OKTOBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here