katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia akifungua kikao Cha mapitio ya sera ya mifugo ya mwaka 2006.
Baadhi ya washiriki wa kikao Cha mapitio ya sera ya mifugo kutoka kanda ya Kaskazini.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi, Dokta Asimwe Rwiguza akiongea katika kikao Cha mapitio ya sera ya mifugo.
Dkt Moses Ole Neselle mtaalamu wa mnyororo wa thamani wa mifugo kutoka FAO akiongea katika kikao cha mapitio ya sera ya mifugo.
Dr Peter Njau mmoja wa wadau wa mifugo kanda ya Kaskazini akiongelea namna ambavyo mifugo Ina mchango katika nchi
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Shirika la chakula na kilimo (FAO) kwakushirikiana na wadau mbalimbali wa mifugo kanda ya Kaskazini wamefanya mapitio ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya mifugo ya mwaka 2006 ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa takribani miaka 15 na kuleta mafanikio.
Akifunfungua kikao hicho katibu tawala wa mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia alisema kuwa,mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa mchango wa sekta ya mifugo kwenye pato la taifa kutoka wastani wa Trilioni 1 mwaka 2006/07 na kufikia wastani wa shilingi Trilioni 10.6 mwaka 2020/21ambapo kwa mujibu wa takwimu kutoka ofisi ya takwimu ya taifa kwa mwaka 2021 pato la Taifa ni 148.5 Trillioni.
Dkt Kihamia alieleza kuwa kati ya mwaka 2006/07 na 2020/21 idadi ya mifugo imeongezeka kutoka ng’ombe milioni 18.5 hadi milioni 33.9, mbuzi kutoka milioni 13.1 hadi milioni 24.5, kondoo kutoka milioni 3.5 hadi milioni 8.5 huku kuku milioni 30 hadi milioni 87.7 jambo linaloonuesha mafanikio makubwa.
Sambamba na e pia alieleza kuwa kumekuwepo kwa ongezeko la idadi ya viwanda vya kusindika maziwa kutoka viwanda 22 mwaka 2005/06 hadi viwanda 105 mwaka 2020/21 ambapo kwa kanda Kaskazini wanajivunia kuwa na viwanda vikubwa vya kusindika mazao ya mifugo ikiwemo viwanda vya kusindika maziwa pamoja na kuwepo kwa machinjio ya kisasa katika maeneo mengi
“Mafanikio hayo katika sekta ya mifugo yamechangia kuwainua wananchi kiuchumi na kuchangia upatikanaji wa malighafi katika viwanda vya kuchakata na kusindika mazao ya mifugo na kuwezesha biashara ya mifugo na mazao ya mifugo ndani na nje ya nchi,”Alisema Dkt Kihamia.
Alifafanua kuwa pamoja na uwepo wa mafanikio pia Kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mifugo mojawapo ikiwa ni kasi ndogo ya wafugaji kupokea na kutumia teknolojia bora za uzalishaji mifugo zinazoendana na wakati ili kuongeza tija ,uhaba wa miundombinu ya ukusanyaji, maji kwa ajili ya mifugo na uwepo wa watoa huduma na pembejeo za mifugo wasiokidhi ubora na viwango vya kitaalamu
Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi,Dokta Asimwe Rwiguza alisema kuwa kikao hicho kimeshirikisha wadau kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Tanga,na Manyara ili waweze kuchangia mawazo yao na uzoefu katika utekelezaji wa sera ya taifa ya mifugo ya mwaka 2006 ambapo serikali imeweka utaratibu wa kuwa na sera ili kutoa mwongozo wa maeneo ya kufanyiwa kazi kwa pamoja kati ya serikali na sekta binafsi na hivyo kufikia malengo yaliyotarajiwa kwa maendeleo ya sekta husika.
“kupitia kikao hiki na vikao vingine vya kikanda vitakavyofanyika mwakani mwezi januari na febuari,wadau wa sekta ya mifugo watapata nafasi ya kutoa uzoefu wao katika utekelezaji wa sera iliyopo,na kuainisha changamoto za kisera wanazokutana nazo kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza kati ya mwaka 2006 na 2021 ili waone uwezekano wa kutatua changamoto hizo kupitia marekebisho ya sera,”Alisema
Aliongeza kuwa katika kufanikisha mapitio ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya mifugo ya mwaka 2006,shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) limeonyesha nia ya kushirikiana na wizara kwa kutoa msaada wa kifedha na kitaalamu ili kufanikisha zoezi hilo.
Naye Dkt Moses Ole Neselle mtaalamu wa mnyororo wa thamani kutoka wa mifugo kutoka FAO alisema kuwa ni kipaumbele chao kufanya kazi na Jamuhuri ya muunganao wa Tanzaniakatika maeneo matatu ambayo ni kilimo mifugo, kilimo mazao na kilimo rasilimali asili ambapo wanaona mifugo inaweza ikatoa tija kubwa kwa maendeleo ya nchi ambapo watashirikia na serikali mpaka pale watakapopata sera nzuri itayohakikisha wapo katika uchumi wa kati.
Mmoja wa wadau walio shiriki katika kikao hicho Dr Peter Njau alisema kuwa kanda ya Kaskazini ni kanda yenye mchango mkubwa sana katika sekta ya mifugo na fursa nyingi zimetokea huko ambapo kanda hiyo ndio Ina watu wanaokaa na makundi makubwa ya mifugo wakiwemo wamasai ambao wameweza kuleta tija kubwa katika nchi hivyo serikali iwasaidie kufanya shughuli hiyo ya ufungaji kwa maendeleo endelevu.