Na Mwandishi Wetu
“Ngoja niseme hili najua wapo ambao hawatanielewa, kwa jinsi unavyoimba na kukaa kwenye key hakuna msanii yeyote katika ‘top five’ ya sasa ya Bongofleva anayeweza kukufikia,” ni kauli ya mtu ambaye kwa miaka 28 mikono yake imetengeneza baadhi ya “biti” kali na za kihistoria za muziki nchini mtayarishaji mkongwe ambaye masikio yake yamesikia sauti nyingi za wasanii waliotoka wakawa maarufu kuliko na walioishia studio, si mwingine bali ni P’ Funky.
Hiyo ni kauli inayoweza kuonesha vipaji ambavyo nchi hii inavyo kitaa na jana vilipata fursa kuonekana kwenye platform kubwa iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Taifa Cup Music Challenge.
Kwa upande wa Bongofleva wasanii 10 waliowakilisha mikoa yao walingia fainali na kwa upande wa Singlei wasanii wanne waliingia fainali kusaka washindi watatu. Matokeo yakawa hivi kwa jina na mkoa husika:
Washindi wa Singeli:
1st Hamza Juma Hamza – Morogoro
2nd Abdulkadri Mwana Kwangaya- Dsm
3rd Saleh Abas Zuber – Mjini Magharibi
Muziki wa kizazi kipya:
1st Abisai Kassanga – Pwani
2nd Meshack Ngemela- Mbeya
3rd Asma Athuman na Asnath Athuman- DSm.
Kwa upande wa soka, netiboli na riadha mashindano hayo yanafikia Tamati leo mchana na jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Credit – Fullshangwe Blog.