NA: Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
SERIKALI imepiga marufuku tabia ya wakurugenzi wa halmashauri chini kuwashusha vyeo walimu wakuu wa shule pindi shule zao zinapopata matokeo mabaya.
Marufuku hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, wakati akifungua mkutano wa wakuu wa shule za sekondari nchini katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mkutano huo wa siku tatu umeratibiwa na Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Umoja wa Walimu Wakuu Shule za Sekondari (TAHOSSA).
Mhe. Ummy alisema inashangaza kuona walimu wakuu wakishushwa vyeo holela na wakurugenzi kila shule inapofanya vibaya wakati mwalimu huyo hajawezeshwa.
“Walimu mmekuwa msaada mkubwa sana kwa maendeleo ya elimu lakini hii tabia ya kuwaonea kwa kuwashusha vyeo imeshamiri na siikubali. Sasa kuanzia sasa sitaki kusikia tabia hii nitawalinda walimu wangu dhidi ya unyanyasaji wa mtu yeyote,” alisema Mhe. Ummy.
Mtoto anapofeli sio tatizo la Mwalimu tu kila mmoja wetu anajukumu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata matokeo bora mwalimu, mlezi/mzazi, jamii wote tunahusika sasa kwanini ahukumiwe Mkuu wa shule tu alihoji Mhe. Ummy.
Na Mkurugenzi unapomvua madaraka Mkuu wa shule je yeye ametekeleza majukumu yake amemuwezesha Mkuu wa shule hiyo ipasavyo; Naomba kwa pamoja tushirikiane katika kuboresha matokeo ya wanafunzi na sio kuadhibiwa mtu mmoja tu.