Home LOCAL HALMASHAURI YA WILAYA MADABA YAKAMILISHA UJENZI WA MADARASA KWA ASILIMIA 100

HALMASHAURI YA WILAYA MADABA YAKAMILISHA UJENZI WA MADARASA KWA ASILIMIA 100


Baadhi ya vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya wilaya Madaba mkoani Ruvuma vilivyojengwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano ddidi ya Uvico-17 ambapo kujengwa kwa vyumba vya madarasa vimesaidia sana kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.

baadhi ya viti na meza vikiwa vimekamilika kwa ajili ya matumizi ya watoto(Wanafunzi)wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika muhula wa masomo 2022 katika shule mbalimbali za sekondari Madaba.
Picha zote na Muhidin Amri

Na: Muhidin Amri, Madaba

HALMASHAURI ya wilaya ya Madaba wilayani Songea, imekuwa ya kwanza kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 katika mkoa wa Ruvuma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Mohamed alisema,Halmashauri hiyo ilipokea jumla  ya Sh. 720,000,000 kutoka Serikali kuu kati ya hizo Sh 730,000,000 kwa ajili ya miundombinu ya elimu na tayari wamejenga na kukamilisha vyumba 17 vya madarasa.

Alisema, katika sekta ya afya wamepokea Sh.390,000,000 ambapo Sh.300,000,000 zitatumika kujenga jengo la dharura na Sh.90,000,000 kwa ajili ya kujenga nyumba tatu za watumishi.

Aidha alisema, mbali na fedha hizo Halmashauri imepokea Sh. 15,851,075 kwa ajili ya uhamasishaji wa chanjo ya Covid-19 na kati ya hizo Sh.6,514,747.00 kwa ajili ya ufuatiliaji.

Ameishukuru Serikali,kwa kutoa fedha hizo ambazo zitaimarisha na kuboresha huduma za afya na miundombinu ya elimu hasa ikizingatia kuwa,Halmashauri hiyo ni ndogo na yenye vyanzo vidogo vya mapato hivyo kwa sehemu fulani kuhitaji ruzuku ya fedha kutoka serikalini na wadau wengine wa maendeleo.

Kwa mujibu wa Sajidu,changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo ni kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi kama bati na saruji,gharama za kusafirisha vifaa kuwa kubwa.

Sajidu, amewaomba wanafunzi na walimu waliofikiwa na miundombinu hiyo katika shule zao kuhakikisha wanatunza ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo kwani fedha zilizotumika ni nyingi ambazo zingeweza kupelekwa kwenye sekta nyingine.

Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Madaba,wamempongeza Rais Samia Hassan kwa uamuzi wa kutoa fedha kwa ajili ya mpango wa maendeleo  na ustawi wa Taifa na mapambano ya Covid-19.

John Danda alisema, jambo lililofanywa na Rais Samia ni la kuigwa na viongozi wengine wa nchi kwani ameonesha uzalendo na uaminifu mkubwa kwa nchi na Watanzania kwa jumla.

MWISHO.

 

Previous articleSERIKALI YAFUNGA MACHINJIO YA PUNDA KWA HOFU YA KUPOTEA KWA MNYAMA HUYO
Next articleTMDA YATOA ELIMU KWA UMMA KUHUSU UDHIBITI WA TUMBAKU RUKWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here