Home LOCAL MIZENGO PINDA ANONGESHA MKUTANO WA WADAU WA DEMOKRASIA

MIZENGO PINDA ANONGESHA MKUTANO WA WADAU WA DEMOKRASIA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Sheikh Alhad Mussa pamoja na viongozi wengine wa dini ya Kiisalam wanaohudhuria mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa unaoendelea Jijini Dodoma. Mkutano huo wa siku tatu unafikia tamati kesho na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.


Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Juma Khatibu(kulia) na Profesa Rwekaza Mukandala Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es –Salaam mstaafu. Pinda ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaohudhuria mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa unaoendelea Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Hazina.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Kapteni (mstaafu) George Huruma Mkuchika akiteta jambo na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais (mstaafu) Jaji Joseph Warioba na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (mwenye kofia), Joseph Butiku wakati wa mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa unaoendelea Jiji Dodoma. Kwenye mkutano huo wa siku tatu wadau wa demokrasia ya vyama vingi watajadili masuala yanayohusu tasnia ya siasa kwa mustakabali mwema wa taifa. (Picha na ORPP)


Previous articleUPASUAJI WA KUZIBUA MSHIPA WA DAMU WA MOYO WAFANYIKA KWA NJIA YA TIBA MTANDAO
Next articleKATIBU MKUU KILIMO ATOA MIEZI MIWILI KUKAMILISHWA KWA UJENZI WA MAABARA YA SUMU KUVU KIBAHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here