Home LOCAL TMDA YAMNASA MTUHUMIWA WA MTANDAO WA UTENGENEZAJI DAWA BANDIA ZA BINADAMU

TMDA YAMNASA MTUHUMIWA WA MTANDAO WA UTENGENEZAJI DAWA BANDIA ZA BINADAMU

Maafisa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wakiangalia Dawa bandia baada ya kumkamata mtuhumiwa anayetengeneza Dawa hizo William Mwangile usiku wa April 14, 2023 nyumbani kwake Kipawa, Jijini Dar es Salaam. 

Mkaguzi wa Dawa wa TMDA Kanda ya Mashariki, Japhari Mtoro akizungumza na waandishi wa habari kuelezea kukamatwa kwa mtuhumiwa wa Dawa hizo.

DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Mashariki inamshikiria mtu Mmoja anayejulikana kwa jina la William Japheth Mwangile (39) mkazi wa Kipawa Jijini Dar-es-Salaam, kwa tuhuma za utengenezaji na usambazaji wa Dawa bandia.

Akizungumza kwenye oparesheni maalum iliyofanywa na Mamlaka hiyo. Mkaguzi wa TMDA Kanda ya Mashariki, Japhari Mtoro amesema kuwa wamemkamata Mtuhumiwa huyo kwa tuhuma za kuzalisha na kusambaza Dawa bandia kinyume cha sheria ya Dawa na Vifaa Tiba kifungu cha 76  sura ya 219.

“Mtuhumiwa amepatikana Aprili 14 mwaka huu, na kutafutwa kwa Mtuhumiwa ni kutokana na kukamatwa  kwa baadhi ya Dawa alizokuwa amezisambaza na baadhi ya washirika ambao amekuwa akishirikiana nao, TMDA imekwisha wakamata wote na aliyekuwa amebaki ni yeye.

“Kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa pamoja na jeshi la Polisi tulifika nyumbani kwa Mtuhumiwa na tukafanya upekuzi tulibahatika kubaini mambo mbalimbali ikiwemo aina mbalimbali ya Lebo za Dawa zikiwa tayari zimeshaandikwa yaani ‘printed levels’ ambazo jumla yake ni 537. Mfano wa hizo Dawa ni quinine sulfate, erythromycin, na aina mbalimbali za Dawa.

“Lakini pia tulikuta viroba vitatu vya unga, kimoja kina unga wa njano na viwili vina unga mweupe unaodhaniwa kuwa ni Malighafi za kutengeneza Dawa, lakini pia tumekuta makopo 12, matupu ambayo ndio yanatumika kuzalisha na kufungasha hizo Dawa na mara baada ya kukamilisha upekuzi usiku wa kuamkia Aprili 15, tulikwenda nyumbani kwa wazazi wa Mtuhumiwa kwa ajili ya kupekuwa pia. amesema mtoro.

Aidha ameongeza kuwa katika Oparesheni hiyo walibaini  uwepo wa vitu mbalimbali ikiwemo mifuko mitupu na Lebo ambazo jumla yake ni 142 ambazo zinafanya jumla ya Lebo zilizokamatwa kuwa 679, nakwamba baada ya kumpata Mtuhumiwa huyo ataunganishwa na wale ambao tayari walishakatwa kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

“Kama mnavyofahamu dawa bandia huu ni uhalifu dhidi ya binafamu ni unyama na ukatili wa hali ya juu kwa sababu anazalisha dawa ambazo pengine ndani hazina kitu,mgonjwa anatumia akitegemea atapona lakini anakutana na dawa bandia Kuna uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa ndio maana hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya atakayethibitika kujihusisha kwa namna yoyote Ile ya uzalishaji ma usambazaji wa dawa bandia.

“Nitumie fursa hii kusema kuwa Serikali Ina mkono mrefu na kutoa onyo kwa wote wanaojihusisha aache mara Moja hatua Kali itachukuliwa kwa yoyote atakayebainika,pia Wananchi haya mambo yanafanyika katika mitaa yetu naomba tutoe ushirikiano kwa jeshi la polisi na TMDA waje kwenye ofisi Siri zitalidwa na hawatakuwa hatarini,” ameongeza Mtoro.

Kwa upande wake Mjumbe wa shina namba 6 mtaa wa Matembele ya kwanza maarufu Matembele Lodge, Maryglory Mambo aliyekuwa akishirikiana na TMDA na jeshi la Polisi kwenye upekuzi huo, ameomba wananchi kuendelea kushirikiana  na TMDA kutoa taarifa za kufichua hali kama hiyo ya watu wanaotengeneza Dawa bandia.

Previous articleMATOKEO YA SENSA YAMEONESHA TANZANIA IMEPIGA HATUA KIMAENDELEO-MAJALIWA
Next articleTUNA MATARAJIO MAKUBWA NA STAMICO- KAMATI YA BUNGE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here