Picha ya Maktaba |
Na: Lucas Raphael,Tabora
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya ambaye anakabiliwa na kesi ya Madai ya fidia ya shilingi milioni 140 jana aliondolewa eneo la Mahakama na askali wa jeshi la polisi akikwepa kamera za waandishi wa habari
Mara baada ya Mahakama kuhairisha shauri lake majira ya saa 09: 49 Asubuhi Komanya alishindwa kutoka nje ya jengo la mahakama kwa saa kadhaa akikwepa kupigwa picha na waandishi wa habari waliokuwepo kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.
Komanya ambaye alifika mahakamani hapo majira ya saa 08:56 akiwa na gari aina ya DSUTA yenye namba za usajiri T 500 DFY rangi nyeusi alikaa ndani ya jengo hilo la mahakama hadi saa 12:42 mchana akiondolewa na askali wa jeshi la polisi aliowaita kumuokoa.
Mahakama ya Wilaya ya Tabora Imeahirisha hadi desemba 27/2021 shauri hilo la Madai hadi Desemba 27/2021 ililiapangiwe Hakimu wa kulisikiliza katika hatua ya Usuluhishi.
Uamzi huo umefikiwa na hakimu Mkazi wa Wilayaya Tabora Nzige Sigwa baada ya kusilikiza maelezo ya makubaliano ya pande mbili kupitia kwa mawakili wao.
Shauri hilo inaonekana kuwa na mvuto wa aina yake kwani baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Tabora wakiongozwa na Mbunge wa Zamani wa jimbo hilo Ismail Aden Rage walifika kusikiliza hatma yake.
Mdai Alex Ntonge kupitia kwa wakili wake Kelvin Kayaga aliiambia Mahakama kuwa anatarajia kuleta Mashahidi wasiopungua Saba huku Komanya akiwakilishwa na wakili Justine Sikon akidai kuleta mashahidi sita wa utetezi.
Shauri hilo dhidi ya Komanya Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora ambaye Uteuzi wake ulikoma juni 19 mwaka huu baada ya kuenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan limefunguliwa na Alex Ntonge mkazi wa Mjini hapa.
Ntonge alifungua kesi hiyo ya madai akitaka alipwe kiasi cha shilingi milioni 140 kama fidia kutoka na vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa na Komanya wakati akiwa ni Mkuu wa Wilaya.
Mdai katika Shauri hilo kupitia kwa wakili Kayaga anadai alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa na Komanya Januari 05/2021.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo Komanya ambaye wakati huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askali wa jeshi la Polisi walifika nyumbani kwake na Kumdhalilisha.
Aliongeza kuwa siku hiyo akiwa na askali wenye Silaha baada ya kufika nyumbani hapo walimkamata mdai Ntonge na kisha walimfanyia vitendo vinavyodhalilisha utu wake mbele ya familia yake na majirani zake.