Home LOCAL SERIKALI IPO PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI KUPINGA VITENDO VYA USHOGA -WAZIRI...

SERIKALI IPO PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI KUPINGA VITENDO VYA USHOGA -WAZIRI NAPE

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya habari, Nape Nnauye akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa Tamasha la Pasaka lililofanyika April 9,2023 katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar-es Salaam.

Kiongozi wa Kiroho wa Huduma ya Inuka Uangaze Mtume Boniface Mwamposa akiongoza Maombi maalum ya kuliombea Taifa na kumshukuru Mungu kwa uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili na kumuombea afya njema ili aendelee kutimiza majukumu yake.

Maelfu ya wananchi waliojitokeza katika tamasha hilo wakifanya maombi ya kumuombea Rais Samia yaliyokuwa yakiongozwa na Mtume Boniface Mwamposa.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM.

Serikali imesema ipo pamoja na viongozi wa Dini katika kukemea na kupiga vita vitendo viovu dhidi ushoga, usagaji na mapenzi ya jinsia Moja, nakwamba vitendo hivyo havina nafasi katika nchi ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya habari, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa Tamasha la Pasaka lililofanyika April 9,2023 katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar-es Salaam.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita haitaruhisu vitendo vya ushoga, usagaji, mapenzi ya jinsia Moja ambavyo kwa sasa vimezua mijadala katika maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania, Afrika , na Duania kwa ujumla.

“Sisi kama Serikali kupitia Raisi wetu tupo pamoja na viongozi wa Dini katika kukemea vitendo viovu,  niwahikikishie hatutapelekwa kwenye utamaduni wa kigeni, tutasimama na tamaduni zetu hatutafungua milango ya laana. alisema Waziri Nape.

Ameongeza kuwa Taifa la Tanzania linaheshimu misingi ya utu na tamaduni zake ambazo zimekuwa zikisimamia maadili ya jamii husika na wananchi wake kwa ujumla.

Kwa upande wake Muandaaji wa tamasha hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema tamasha hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuishukuru Serikali kwa kazi nzuri iliyofanyika katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluh Hassan.

“Serikali imefanya kazi kubwa sana katika kipindi hiki cha miaka miwili hivyo tumeona tumshukuru Mungu kwa hilo na kuendelea kumuombea Rais wetu awe na afya njema na kuendelea na majukumu yake ya kuijenga Nchi na tuendelee kumuunga mkono.

“Na kama mnavyoona Tamasha letu ni la bure kabisa na limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na tumefanya maombi na wachungaji wameliombea Taifa hapa akiwemo mchungaji Mwamposa na wengineo” amesema Msama.

Maombi maalum ya kuliombea Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aweze kuwa na afya njema na kufanya majukumu yake vizuri yameongozwa na Kiongozi wa Kiroho wa Huduma ya Inuka Uangaze Mtume Boniface Mwamposa ambapo pamoja na maombi hayo amewasihi Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika Jitihada zake za kupambana na vitendo viovu vinavyotaka kuliharibu Taifa.

Tamasha hilo la bure lilihudhuriwa na maelfu ya watu ambapo kwaya mbalimbali zimemtukuza Mungu kupitia nyimbo zao ambapo waimbaji wote walioalikwa walihudhuria.

(MATUKIO MBALIMBALI KATIKA TAMASHA HILO)

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 10,2023
Next articleRAIS SAMIA APONGEZWA KUCHUKUA HATUA RIPOTI YA CAG
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here